Ilikuwa tarehe kama ya leo january 2011

marejesho

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
6,635
Reaction score
3,656
Tarehe kama ya leo, mwezi wa kwanza, mwaka 2011 (6th Jan 2011), Nilipata fursa ya kujiunga na Jamii Forums. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kudumu humu jamvini mpaka sasa ..

SABABU YA KUJIUNGA
Habari za SIASA motomoto nilizokuwa nikizipata miaka ile kwenye JAMBO FORUMS, ndizo zilikuwa chachu ya mimi kujiunga tena...

KWA NINI TENA?
Baada ya kukaa nje ya mtandao kwa muda mrefu, nadhani Jambo Forums waliondoka na password yangu... Nilijaribu sana kukumbuka password lakini niliambulia patupu...."Sikuwahi kupata wazo la kuwauliza Mods"

MAFANIKIO
Nimeweza kupata marafiki wengi ,ambao tunafurahi pamoja, tunashirikiana katika mambo mbalimbali.Kimsingi wamekuwa ni sehemu ya familia yangu....
Lini ningekwenda Tanga na kuenjoy kiviile kama sio JF? Big Up sana Arusha-WING, TA-WING na DAR-WING....

Nimeweza kufuatilia mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea Nchini,ya kupendeza,kuhuzunisha nk.... Daima nitashukuru kuwepo kwa Jukwaa la Siasa maana bila wao, hakika nisingefika hata huku Chit Chat....

SHUKRANI ZA PEKEE.

Ziwafikie Mods ambao mpaka sasa hawajawahi kunipa hifadhi kule BAN GUEST HOUSE... Nasikia kule kuna mateso balaa, alinidokeza Mungi . Muendelee na moyo huo huo, mkizidi kufanya kazi yenu kwa umakini, msinikumbuke kabisa katika huo ufalme wa BAN..

Pili kwa mume mpenzi Filipo ,kwa kunidaka juu juu.. Nakiri kwamba upinzani upo ,tena mkubwa toka kwa Smile , ladyfurahia , sweetlady Arabela amu ila sintolala usingizi kabisa.... Baadhi ya niliowataja kwa namna moja wanampenda au wanapendwa na mume wangu.... Nayahesabu kwamba ni mapungufu ya kibinadamu....
UJUMBE:
Mimi na Filipo hatukukutana barabarani ,na kama hamuamini angalieni lini tulijiunga JF....


Nawatakia Upendo, Furaha , na Mafanikio katika kila Jambo mtakalolipanga kwa mwaka huu mpya 2013...

Copy: PakaJimmy , Blaki Womani , Preta , Lily Flower , Arushaone , Mr Rocky , Mungi , Mzee wa Rula , LiverpoolFC , Erickb52 , Smile , Arabela , Dark City , madame V , Nicas Mtei na wengine ambao sijawataja...
 
Last edited by a moderator:
Ingawa hujani mensheni hapo juu, ila nilivyouona mwandiko tu wa hedingi nikajua huyu ni best yangu lazima niingie humu.
Karibu JF kwa mwaka mwingine mpya tena...
 
Ingawa hujani mensheni hapo juu, ila nilivyouona mwandiko tu wa hedingi nikajua huyu ni best yangu lazima niingie humu.
Karibu JF kwa mwaka mwingine mpya tena...

Oh noo... watu8 wewe nilikutag ila inaelekea kuna kitu sijakifahamu vizuri..... Ntaomba nikija Dar unifundishe kutag zaidi ya mtu mmoja...

Tuko pamoja best yangu....
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana siri kubwa ya wewe kutofika kijiji cha mateso cha mjini BAN ni uvumilivu wako na busara ulizo nazo happy birthday marejesho mungu akupe miaka mingine mingi hapa jf.
 
Last edited by a moderator:
Happy birthday jf marejesho...
Ila ujumbe kuhusu mume wako umenitachi sana.
Naomba nikupe list kwenye upinzani Paloma kaongezeka tena your hubby Filipo kamuambia amemkatia fast jet aje a town asuke yeboyebo na amnunulie white dresss.
Pia kuna Lusile japo kaja kivingine mumeo nae anazengea...
Pole shostito
 
Last edited by a moderator:

We mwana we tartiibu, ya nini kuntia pressure mwenzio!???
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana marejesho...

Wewe ni miongoni mwa watu ambao siwezi kujutia kuwafahamu...huu ni ukweli kutoka kwa Babu na Bibi pia!!

Sijui ni kwa sababu wewe ni dot com na mimi ni wa 1947, ila sijapenda uandishi wako kabisa...nilitamani niache kusoma ujumbe wako. Kama siyo uvumilivu wa kiutu uzima, ningekutwangia simu na pangechimbika...tangu lini mtu unamtaja mume wako mpenzi anayekuweka kwenye hii dunia kwa yale mambo ya teacher gfsonwin mwishoni mwa barua??

Hapa namshauri Filipo akate rufaa ili uandike upya...ila sitamruhusu atishie talaka kwa sababu list uliyoitaja ya watu wanaomezea mate mgodi wako inatisha...

But...you are such a wonderful lady (mimi ni mtu mzima, retired MG na nina uzoefu wa miaka kibao, sihitaji kusema zaidi ya hayo) and JF is blessed to have you onboard....

Huu ujumbe nautuma kwa Invisible, Maxence Melo and the crew.....wakiweza kuattract JF members 10,000 kama wewe watajiendea kupumzika....

Kila la heri na uendelee hivyo hivyo......Hapa babu kamwaga baraka zote....!!


Babu DC!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…