Ilikuwaje Azimio la Arusha likafutwa Zanzibar, kwenye kikao kilichofuata baada ya Nyerere kutoka?

Ilikuwaje Azimio la Arusha likafutwa Zanzibar, kwenye kikao kilichofuata baada ya Nyerere kutoka?

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Posts
1,334
Reaction score
989
Ukittafakari mfululizo wa kalenda na matukio, basi inawezekana kuna jambo ambalo hatulijui.

Mwalimu Nyerere aliachia uenyekiti wa CCM, Friday, August 17, 1990 huku Mkutano mkuu wa CCM ukiwa kikaoni.
Mkutano huo ndiyo ulimuweka mwenyekiti mpya, Ali Hassan Mwinyi na katibu akawa Horace Kolimba. Lakini mkutano huo pia, ndiyo uliompitisha Salmin Amour agombee urais Zanzibar kwa mara ya kwanza.

Hivyo, mkutano ulipoisha, shughuli iliyofuata ni pilika za uchaguzi uliofanyika Zanzibar, Sunday, October 21, 1990 na Bara ukafanyika, Sunday, October 28, 1990.

Zikafuata pilika za kuchagua cabinets kwenye mwezi November, na baada tu ya cabinets, zikafuata pilika za haraka za Waziri mpya wa mambo ya ndani aitwaye Augustine Mrema ambaye ndani ya mwezi mmoja alishatoa amri zaidi ya nne za majukumu yatekelezeke ndani ya siku saba.

Kiserikali, tukio kuu lililofuata ni sherehe ya Mapinduzi Zanzibar yaani January 12, 1991.

Tukio lililofuata ndilo limenifanya niandike post hii, nalo ni NEC ya CCM kukutana Zanzibar kuanzia February 14, 1991. Utaona kwamba hiki ndicho kikao cha kwanza kichama baada ya mkutano ule aliong'atuka Nyerere yaani siku 181 tu tangu Nyerere aachane na uenyekiti.

Ni wazi kwamba agenda kuhusu uchaguzi ingeweza kuwemo kwenye kikao hiki. Kwa ujumla kikao hiki ni cha kihistoria kwa CCM yaani ndicho kikao cha kwanza Nyerere akiwa si mwanasiasa.

Sasa, kikao hiki cha kwanza Nyerere akiwa si mwanasiasa kiliongelea nini? Kikao hiki ndicho wengi husema kiliua Azimio la Arusha na kikapewa jina Azimio la Zanzibar. Mtakaojadili na kuingia sana kuhusu kuaawa Azimio la Zanzibar mimi si hoja yangu.

Mimi hoja yangu ni kunisaidia kujiuliza na kupata majibu kwamba, kulikuwa msukumo gani ambao ulisubiri tu Nyerere aondoke madarakani halafu Azimio lake la Arusha lifutwe kikao kinachofuata cha chama. Ajenda za kikao hiki ziliandaliwa lini?

Kama sikosei, ni wazi ajenda za kikao hiki ingewezekana Mwalimu alikuwa anazifahamu kwa kuchukulia kwamba haiwezekani uwe mwenyekiti wa chama halafu usiwe na fununu au dalili za kujua ajenda za kikao kinachofuata ziwe ni za jambo gani.

je, kuna uwezekano kwamba Mwalimu alijua kwamba kikao kinachofuata baada ya Mkutano Mkuu wa August kitakuwa ni cha kufuta Azimio la Arusha? Kama alijua basi binafsi ninaona heri lilifutwa akiwa ameshaondoka, maana sijui angesimamia vipi ajenda hiyo.


Kama mwalimu hakujua ajenda za next meeting, je, walioandaa ajenda, waliwezaje kumficha mwalimu hadi dakika anaondoka kitini, kukafuatiwa na uchaguzi na mambo ya cabinet mpya.

Nasema hivi kwa sababu ajenda ya kufuta Azimio la Arusha haikuwa ajenda ndogo. Nashindwa kuamini kwamba ajenda kubwa kama hii iibuke tu ndani ya mwezi mmoja baada ya taifa kutoka uchaguzini.

Na kama chamani walikuwa wanweza kutunza siri hadi mwalimu asijue, basi ingekuwa busara zaidi walau kusubiri hadi August 1991 ambapo ingekuwa umepita mwaka mzima na vikao kadhaa vya NEC vimeshapita na ajenda zingine walau za kufumbafumba , kuliko kusubiri kikao kinachofuata baada ya Mwalimu kuondoka ndipo makucha yaonekane.

Naamini humu JF kuna wanaoweza kujua zaidi. Narudia, najiuliza speed ya kufanya jambo lile kubwa, lionekane limekuja ghafla, wakati haikuwa rahisi kwa Mwalimu kufichwa jambo kirahisi eti alipoondoka tu kikao kilichofuata kikaamua kusema alhamdulilah paka katoka sasa panya atawale, to hell with Azimio la Arusha.

SAIDIA KUTAFAKARI
 
Kwa mtu anayefikiri vizuri kama Bubu muongeaji, swala la JK I kujua kuwa Azimio la Arusha lilitakiwa kufutwa si jambo la kushangaza, kwa maana pamoja na mambo mengine JK wa kwanza alijua mabadiliko mengi saana ambayo binafsi yeye ingekuwa aibu kuyasimamia. Baada ya mwaka 1978/9, nchi kuyumba kiuchumi kwa vita vya Kagera JK-I hakuwa na miujiza ya kukataa shinikizo kutoka kwa IMF, WB, na NATO(magharibi).

JK kama kiongozi aliyeamini ujamaa mwanzoni mwa maisha yake ya siasa baadae alikuja kuzidiwa nguvu na ubepari wa magharibi na ubepari ndani ya chama chake. Kama kiongozi asiyependa kuonekana kigeugeu alisimamia mabadiliko haya nje ya serikali, alianza na kung'atuka kwa kumuachia Ikulu AHMwinyi lakini akaendelea kukosoa na wakati mwingine kuongoza nchi nje ya Ikulu.

alikuwa kiongozi wa chama tawala wakati ule chama kinachoiongoza serikali, serikali ilifanya yale yaliyoagizwa na CC na NEC, JK akiwa mwenyekiti.

JK katika kuitikia vichocheo vya Magharibi aliamua kuondoka katika madaraka rasmi kwa kumuachia AHM asimamie mabadiliko.
Swala la JK kujua agenda za kikao kilichofuata linatokana na ukweli kwamba alijua ni kwa nini aliachia ngazi, na si kwa sababu alikuwa Mwenyekiti wa chama. Hakuna kitu cha kumuondoa JK katika mabadiliko yaliyotokea katika nchi hii, ila aliyaruhusu na kuondoka madarakani au aliyaruhusu kwa kuondoka madarakani.

Bubu muongeaji anaishia hapo kwa leo. Tusikilize maoni zaidi ya wadau.
 
Kama Azimo la arusha lilivyokufa bila wale waliotembea kwa miguu kuambiwa Ndiyo ilivyo kuvunjika kwa Muungano kwani wale waliobeba mchanga na kuchanganya mchanga hawatapewa nafasi kuutetea
 
Azimio la Zanzibar February 14,1991 hatimaye linaipeleka CCM Kuzimu hapo 25.10.2015 mapema asubuhi.
 
Back
Top Bottom