Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Hakuna ubishi kuwa baada ya kukubali au tuseme kuingizwa mkenge na kupokea dini nyemelezi za kigeni, tulipoteza kila kitu.
Tulipoteza utambuliko wetu, majina yetu, utu wetu, upendo wetu, ushirikiano wetu, dini zetu na kuteuka vikaragosi vya kiimani. Leo watu wanajiita wakristo au waislam lakini si waswahili. Wanachukiana hata kuuana wao kwa wao. Wanaibiana kwa kuuza neno la mungu. Wamegeuka wavivu wa kutofanya kazi wala kufikiri na kutegemea miujiza.
Tumejenga misikiti na makanisa mengi kuliko viwanda na mashule na vitu vingine vya maana. Tulianza kuchukia vitu vyetu na wenzetu na kuabudia vya wageni hadi watu wanaapia miji ya watu utadhani hawana miji.
Tulifundishwa utakatifu feki unaowatukuza washenzi waliotuuza na kututawala. Walitwambia tusiibe, wakatuibia. Walisema tusidanganye wakatudanganya. Walisema tusie, wakatuua. Walisema tusitamani mali. ya mtu baada ya kutuibia na kutajirika. Walitufundisha kupendana wakati wakituchukia hadi leo. Orodha ni ndefu kweli kweli.
Tumepoteza kila kitu na kuwa watumwa wa dini na waliozibuni na kutuletea. Je ilikuwaje mababu zetu wakakubali ujinga huu?