Ukiachwa hilo ni kosa lako.
Ama umemkubali mtu ambaye si sahihi tangu mwanzo. Kosa lako.
Ama mtu alikuwa sahihi mwanzo akabadilika, ukashindwa kumuacha wewe kwanza. Kosa lako.
Ama mtu sahihi, ila kakuchoka tu. Kosa lako.
Vyovyote vile hutakiwi kuachwa.
Ukiachwa usilalamike. Tafuta mwingine tu.
Kwa sababu, kuachwa ni kosa lako.
Bila kujali wewe ni mwanamke au mwanamme. Bila kujali unahudumia au unahudumiwa.
Unatakiwa kuwa na mvuto mkali sana kiasi kwamba wewe tatizo lako liwe ukiingia kwenye mahusiano watu hawataki kuachana nawe.
Yani wao ndio wawe wanalazimisha mahusiano na wewe, sio wewe unalazimisha mahusiano na wao.
Ukiachwa ujue ushazembea sehemu hapo.
Jitafute ujiongeze mwenyewe bila kutaka kumdhuru mtu.
Credit to
Kiranga