ITEGAMATWI
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 5,340
- 4,086
- Thread starter
-
- #21
Hii inatikana na wakati gani siku huanza kwa wenzetu. Kwa wao siku mpya huanza saa sita na dakika moja usiku (00:01) kwa hiyo saa moja asubuhi ni masaa saba (7.00 Anti Meridian) tangu siku ianze.
Kwasisi waswahili siku huanza jua linapochomoza, kwahiyo saa moja asubuhi ni lisaa limoja tangu jua lichomoze (saa 12 asubuhi). Tulifanya hivyo kwasababu katika ukanda wa ikweta tuna masaa 12 ya mwanga na 12 ya giza, mwaka mzima. Wenzetu wasinge weza kutumia kigezo cha jua kwakuwa muda wa jua kuchomoza na kuzama hubadilika kutokana na majira
Asante sana Mkuu kwa mafahamisho. Bado kuna uwezekano kuwa neno *gari limetokana na *car, hasa ikiwa gari limeingia katika Kiswahili kutoka Wahindi ambao wao kama sisi tulikuwa makoloni ya Mwingereza. Maneno baba (papá) au mama (mamá) nilikuwa ninafikiri yametokana na kilatini.Sahihisho........gari ni neno linalojitegemea na tumekopa kwa wahindi...just like baba
kuna vitu vyengine havizingatii sheria wala kufata nasaba...ila wazo hili la GOODRICH nalikubali .
waingereza na wafaransa wanaiita moroko ,ila wenyewe wanaiita MAGHRIB, Je pana uhusiano wa majina hayo ?? Zamani Uholanzi ilikuwa ikijulikana sana kwa jina la Udachi, ila wao wenyewe hawalifahamu neno hili kwani lina nasaba na ujerumani na sio wao.