Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!




Baba wa 3 hili swali ndilo hadi muda huu linaniumiza kwamba alienda kufanya nini pale .Ila napata jibu kwamba alienda Dodoma eneo la Dodoma kuvunja record yake mwenyewe ya kuhutubia muda mrefu zaidi kwa kusema mzaha kwa watanzania
 
Matumaini na mwelekeo wa mtanzania kwa raisi kikwete yamefika mwisho. Kikwete ameshindwa kufikiri , kutenda na ameambatana na uchumi wa kiswahiba na kukosa kabisa mapenzi na nchi yake. Kama alivyoliacha Jimbo lake la uchaguzi likiwa hoi baada ya kukaa bungeni takribani miaka kumi na ushee atawaacha watanzania wakiwa wamechoka kuliko kipindi chochote ktk maisha ya Mtanzania.
Kikwete ameshindwa uongozi kura ya kutokuwa na imani naye ipigwe. Au awe muungwana aachie ngazi mwenyewe.
Ni Tanzania pekee Raisi anakula deal na wezi, wahujumu na walarushwa.
Hotuba yenye kichefu chefu iliyoandikwa na hulka ya kifedhuli inaonyesha Tanzania iliyokufa.
Kauli mbiu ya Kikwete: Nguvu mpya wizi mpya, utetezi wa ikulu ndio dira ya ikulu ya kikwete.
 

Maneno mazito na yaliyojaa kila chembe ya ukweli mkuu!!!!
 
.



Jakaya Mrisho Kikwete kushitakiwa?!








Kikwete ameashiria kuwasamehe waliohujumu uchumi hata kabla hawajahukumiwa. Kwa kosa hili twaweza kumburuza mahakamani. Raisi huwa anawasamehe ambao tayari wameshahukumiwa.

Kipindi chake cha Urasi kikipita, tunahitaji tu ushahidi uliokaa vizuri. Ole wake!



.
 
Nilisema Hii Hotuba imeleta wahaka kwa uuma wa watanzania........
 
Naomba upunguze munkari mjomba. Kwanza hii hoja ilikuwa haihitaji mada maalum. Wazungu wana msemo fulani: bark is worse than bite. Hebu jiulize: pamoja na ushahidi wote uliyo wazi hakuna Mtanzania hata mmoja kati ya watu milioni 40 (Dr. Slaa na Rev. Mtikila included) aliyeweza kufungua mashitaka mahakamani dhidi ya Mkapa (achilia mbali mhusika mwenzake Daniel Yona). Sasa Kikwete mtamuanzia wapi?
 

Ewalaah! Swadaktaah! Alhamdulilaah! Takbiru alaah walibaahlu! Ila naona umesahau the constructive part of your criticism. Sasa baada ya kunena maneno mazito yenye jazba kubwa kama hayo; jee una ushauri gani kuhusu pendekezo au mapendekezo ya suluhisho la malalamiko uliyo nayo dhidi ya Kikwete na serikali yake?
 

Nchi inaendeshwa na wachawi anaotembea nao Kikwete!!!!!!!
 
Sasa baada ya kunena maneno mazito yenye jazba kubwa kama hayo; jee una ushauri gani kuhusu pendekezo au mapendekezo ya suluhisho la malalamiko uliyo nayo dhidi ya Kikwete na serikali yake?

Jazba ndicho kitu ambacho watawala wanakijenga kwa wananchi wao. Hii inatokana na, pamoja na mambo mengine, kushindwa kusikiliza ushauri ambao umekuwa ukitolewa miaka nenda miaka rudi. Sasa ushauri huo utakaotolewa sasa utakuwa na sura gani tofauti na ushauri uliopata kutolewa huko nyuma?
 
Jamani,

Haya matatizo ni ya Kikwete mwenyewe, CCM culture, au systemic and structural Tanzanian problems?
 

It is possible to start from the bottom to the top.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…