I'm Tanzanian and I beg you to brief me on your decisions to replace KANU

TuntemekeSanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
1,346
Reaction score
862
Hapa Tanzania kuna vuguvugu nyingi za baadhi ya makundi na vyama kutaka kuiangusha CCM na kuweka Vyama Pinzani kwa madai ya kuleta mabadiliko ya mtu/mwananchi wa kawaida na maendeleo mengine kwa ujumla wake.

Je; ninyi mliothubutu kufanya hivyo, mmefikia malengo yenu kwa kiasi gani?(ninyi kama wananchi wa kawaida).

Je; mnadhani mngeendelea kuipigia kelele KANU na kupambana kwa kushirikiana na Viongozi wa KANU ingesaidia na ingekuwa bora zaid kuliko kubadilisha Chama na kuikabidhi nchi kwa Wapinzani?

After that, i would like you comment in "Swahili" rather than English as there have been some Tanzanians visiting your Forum and get troubled with English.

Asanteni sana.
 
Mabadiliko hatungeyapata tungeendelea kutawaliwa na KANU. Kulikuwa na haja kubwa sana kuwatoa madarakani na kuanza upya.
 
Misingi iliyowekwa na TANU/CCM n tofauti kabisa na KANU
Hvyo Ccm itatawala muda mrefu sana
 
Naomba nikuulize wewe uni brief advantage uliyonayo chini ya utawala wa ccm,na je ungetamani kubaki hivyo milele,everything is gonna change at time,as we live and die ccm as KANU too is on the edge of its grave.
 
Hivi hitimisho lake ulimuelewa kakwambia mtumie kiswahili zaid lakin mnang'ang'ania utumwa wa mwingereza mpaka lin
 
Hapa Tanzania kuna vuguvugu nyingi za baadhi ya makundi na vyama kutaka kuiangusha CCM na kuweka Vyama Pinzani kwa madai ya kuleta mabadiliko ya mtu/mwananchi wa kawaida na maendeleo mengine kwa ujumla wake.

Je; ninyi mliothubutu kufanya hivyo, mmefikia malengo yenu kwa kiasi gani?(ninyi kama wananchi wa kawaida).

Je; mnadhani mngeendelea kuipigia kelele KANU na kupambana kwa kushirikiana na Viongozi wa KANU ingesaidia na ingekuwa bora zaid kuliko kubadilisha Chama na kuikabidhi nchi kwa Wapinzani?

After that, i would like you comment in "Swahili" rather than English as there have been some Tanzanians visiting your Forum and get troubled with English.

Asanteni sana.

Kwa maoni yangu binafsi, kweli tumefanikiwa pakubwa baada ya kuiondoa KANU madarakani, kuna mengi tunayoyaona yaani hata ingenyesha mvua ya paka wala panya hatungeyapata chini ya uongozi wa KANU. Kwanza kabisa katiba mpya nzuri ni mfano wa mambo ambayo KANU ilivuruga kabisa na kuhakikisha tunahangaika, ila kwa kuindoa KANU gharama ililipwa na hadi sasa kuna jinsi moja au nyingine tunaendelea kulipa, nchi iligawanyika sana zaidi ya tulivyokua.

Lakini sasa hayo tumejaribu pakubwa kuyarekebisha, nchi sasa inasonga mbele kwa kasi, tunayo katiba mpya, maendeleo tunayaona na mambo mengi ambayo siwezi yaorodhesha hapa.

Tukija upande mwingine, mimi nimefuatilia sana siasa za Afrika Mashariki, Tanzania ikiwemo na kwa kweli upinzani wenu bado mbali sana, sioni uwezo wao wa kuitoa CCM madarakani. Wao wameshindwa kuwahubiria Watanzania nini watafanya tofauti kisichofanywa na CCM. Kuna siku nilihudhuria mkutano wa Chadema ambao hata viongozi wa ngazi za juu walikuwepo, maana napenda siasa sana. Sasa kwenye huo mkutano, kidogo ungedhani ni mkutano wa CCM maana kila aliyepata fursa ya kuongea, alikua anaponda CCM, walitaja sana hicho chama zaidi ya chama chao. Niliwaskiliza kwa makini na hakuna aliyenifanya nione ubora wao.

Hebu angalia UKAWA wanachokifanya sasa hivi, eti wanasusia mchakato mzima wa katiba, badala ya wao kuonyesha mwongozo na kuongoza kwa kuelezea ubaya wa katiba, wao wanajiweka pembeni. Kenya tuliangusha katiba mbaya, viongozi wa upinzani kipindi kile wakiwa aliye rais wa sasa Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Walizunguka nchi na kutuelezea mabaya ya ile katiba. Hawakuogopa na waliongoza kwa mbele na ilipofika kura ya maamuzi, tuliipiga chini. Na hapo serikali ikaelewa kilichokuwa kinazungumzwa, maana tulirudia mchakato na kuhakikisha katiba yenye maoni ya mwananchi imekubalika.
 
Asante kwa uchambuzi yakinifu Mkuu,nina imani umenishibisha. Ngoja niendelee kusubiri wadau wengine humu ndani.
 
Hapa Tanzania kuna vuguvugu nyingi za baadhi ya makundi na vyama kutaka kuiangusha CCM na kuweka Vyama Pinzani kwa madai ya kuleta mabadiliko ya mtu/mwananchi wa kawaida na maendeleo mengine kwa ujumla wake.

Je; ninyi mliothubutu kufanya hivyo, mmefikia malengo yenu kwa kiasi gani?(ninyi kama wananchi wa kawaida).

Je; mnadhani mngeendelea kuipigia kelele KANU na kupambana kwa kushirikiana na Viongozi wa KANU ingesaidia na ingekuwa bora zaid kuliko kubadilisha Chama na kuikabidhi nchi kwa Wapinzani?

After that, i would like you comment in "Swahili" rather than English as there have been some Tanzanians visiting your Forum and get troubled with English.

Asanteni sana.

Ndugu unalinganisha vitu visivyolingana! Kwanza huwezi kufananisha CCM na KANU ilivyokuwa! Na mazingira ya Kenya na Tanzania ni tofauti sana kuliko Mtu unavyoweza kudhania!
Nitajaribu kuelezea, KANU iliweza kuondoka Kenya kwa sababu moja kubwa nayo ni kwamba Kenya Siasa ni Mtu/Watu na SIYO Chama, wakati TZ kwetu Siasa huwa ni Chama, yaani huwa hatufwati Mtu bali tunafwata Chama hivyo ktk mazingira kama hayo utaona ya kwamba Kenya waliweza kuondoa KANU lkn walibadilisha tu jina la KANU kwani wale wale waliokuwa KANU ndio hao hao waliokwenda kuanzisha Vyama vingine na kuviita majina tofauti kila kukicha mara utasikia ODM mtu huyo huyo wa ODM ataondoka na kwenda kuanzisha sijui NARC baadaye akiona huko akieleweki anaenda kuingia JUBILEE nako akiona hakuna maslahi basi atahama na kwenda labda sijui CORD!

Na kwa kuwa basi Siasa za Kenya ni Mtu na SIYO Chama, basi hawa Viongozi huwa wanahama na Watu au wafuasi wao, yaani kwa mfano Raila Odinga wa Kenya watu wake ama wafuasi wake watamfwata popote pale na Chama chochote kile atakachokwenda iwe KANU au sijui CORD na Uhuru au Ruto ni hivyo hivyo!

Kwa hiyo kwa kifupi KANU ya Kenya iliweza kufa au kuondolewa madarakani SIYO kwa sababu eti Wakenya walikuwa wamekichoka HAPANA, iliweza kuondolewa kwa sababu Viongozi wa KANU walifarakana kutokana na Uchu wa Madaraka na hivyo kuwafanya kukihama KANU na kwa kuwa Siasa Kenya ni Mtu na SIYO Chama basi walihama na Watu wao!

Na ndio maana wanaolinganisha CCM na KANU huwa wanafanya kosa kubwa sana, kwani CCM haiwezi kuondoka madarakani kirahisi hivyo na sababu ni kama hiyo niliyoitaja juu halafu kingine Tanzania Raisi wa nchi ndiyo Mwenyekiti wa Chama hivyo ana madaraka makubwa sana kwenye Serikali na pia Chamani, hivyo ingawaje wengi hawataki kuamini hivyo lkn CCM bado ina nguvu sana TZ na itabaki kuwa hivyo miaka mingi ijayo na ushahidi upo wazi ndani ya jiji la Dar kuna Wabunge watano ama sita na kati ya hao wapinzani ni wawili tu na waliobaki ni wa CCM, hivyo kama wananchi wangekuwa hawaitaki CCM basi Dar isingepaswa kuwa na Mbunge wa CCM hata mmoja!
 
limetumbuka
I hope tuko pamoja mkuu. What i'm in search huku, ni just simple research ili nipate ufahamu zaid juu ya kufanya mabadiliko.

Lakini,nakushukuru sana .Umeonvea mambo muhimu na makubwa pia.
 
Last edited by a moderator:
MK254 uko vizuri kumbe wakati mwingine hufanya makusudi tu

Siku zote niko sawa mkuu, tatizo lenu hamjazoea agreeing to disagree, kwamba lazima niendane na kile mnachofuata siku zote. Kubali kuna dissenting voices around you, hata mkeo nyumbani ana uhuru wa kubisha.
 
Hapana lawmaina, mke hana uhuru wa kubisha.
 
Bila kumwaga damu ya walau watanzania 100 hakutakuwa na kuheshimiana na CCM itabakia madarakani milele. Pale Shinyanga 2010 CCM walitumia usalama wa taifa kubadili matokeo ya CHADEMA kuipa CCM na vice versa then wananchi wakabaki wanakata viuno kurudi nyumbani wanaogopa virungu vya polisi. Huwezi kulitoa dubwana kubwa kama CCM limekaa madarakani miaka 50 bila kumwaga damu.
 
mwanaume wa ukweli hatoi wazo bovu bwana dhuks! Ukitoa wazo hadi mkeo alipinge au abishe ku adhere. Go and sit alone and re think about your role and change.
 
na wewe umwage hiyo damu si kusakizia watu huku umejifungia chumbani nyuma ya keyboard
 
Hapana lawmaina, mke hana uhuru wa kubisha.

Aha! sasa ndio hapo, kama humpi mke wako uhuru wa kubisha ataenda kulilia kwenye kifua cha mwanamume mwengine ili "amfariji".
 
Hapa Tanzania kuna vuguvugu nyingi za baadhi ya makundi na vyama kutaka kuiangusha CCM na kuweka Vyama Pinzani kwa madai ya kuleta mabadiliko ya mtu/mwananchi wa kawaida na maendeleo mengine kwa ujumla wake.

Je; ninyi mliothubutu kufanya hivyo, mmefikia malengo yenu kwa kiasi gani?(ninyi kama wananchi wa kawaida).

Je; mnadhani mngeendelea kuipigia kelele KANU na kupambana kwa kushirikiana na Viongozi wa KANU ingesaidia na ingekuwa bora zaid kuliko kubadilisha Chama na kuikabidhi nchi kwa Wapinzani?

After that, i would like you comment in "Swahili" rather than English as there have been some Tanzanians visiting your Forum and get troubled with English.

Asanteni sana.

mkuu, Naona wengi wamechangia sana katika mada huu. Mabadiliko yalikuja ingawa yalikuwa chini sana ukilinganisha na vile tulivyokuwa tukitarajia. Kweli tumepoteza miaka mingi sana.

Kile ambacho ningeweza kukuambia ni kuwa Mwanasiasa usimtegemee sana. Viongozi kama Nyerere waliokuwa wakipenda nchi yao hawapo siku hizi. Baada ya Kibaki kuingi madarakani, kulikuja na filosophia iliyoitwa "It is our turn to eat." Unaweza ukasoma chapter 1 ya hicho kitabu hapa (Chapter 1 ni The Big Man.)

http://theorwellprize.co.uk/wp-content/files_mf/michelawrongitsourturntoeat.pdf
 
Back
Top Bottom