WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
sheria zinatungwa na matajiri kuwazuia maskini kuwasogelea matajiri na kuhakikisha matajiri wanaendelea kuwakandamiza maskini. Zinatungwa ili kuwapa maskini kiinimacho cha utajiri! Mara zote sheria zinatungwa kuwafurahisha matajiri na kuwaridhisha maskini lakini wakati wote kuwanufaisha watawala!
Mpaka sasa wananchi wameweza kuona ni kwa jinsi gani matatizo yanayoikumba nchi yetu yanazidi kuongeza licha ya kuwepo sheria, vyombo na taasisi mbalimbali za kisheria zenye nguvu na mamlaka ya kuyashughulikia.Wapo wenye kuamini kwamba maadam kuna sheria na vyombo hivyo, basi mafisadi watakiona cha moto.Kwani Sheria ni nini, ni za nani na kwa manufaa ya nani?
Sheria ni ile mambo ya kumfunga mama ntilie miezi sita gerezani kwa kosa la kuuza chakula mtaani, na kumwacha fisadi anaingia hadi bungeni, anachangia hoja na inapigiwa makofi. Hii ndo sheria mzee...
... sisi kupitia wabunge wetu tunatunga sheria
Tafsiri mojawapo ya sheria ni:
"Sheria ni chombo cha mabavu cha dola".
Kama ni chombo cha dola tena cha mabavu sisi kupitia wabunge wetu tunatunga sheria na kuwaachia watafsiri sheria, ( mahakama) kuzitumia hizo sheria kwenye kesi/mashauri mbaimbali - ya madai na ya jinai.
Katika kutekeleza sheria kuna vyombo vingi na michakato mingi.Je mwisho wa siku tunapata nini? je ni kweli kuwa tunatunga sheria zenye kuwakilisha matakwa na matarajio yetu? Je, wanaotafsiri hizo sheria, sisi kama wananchi tunawawajibisha vipi? ( nauliza maswali haya ya kifilosofia kuchagiza mjadala)
La hasha.
Bunge letu sio la kutunga sheria bali ni muhuri, rubber stamp, ya miswaada au hoja chovu yeyote ya serikali. Mara ya mwisho wabunge kutunga sheria wenyewe ilikuwa zaidi ya miaka kumi na mbili iliyopita, 1997 ( sheria ya Balozi P. Ndobho, NCCR Musoma Vijijiji, sheria ya A. Mrema, NCCR Temeke, sheria ya J. Mungai, CCM Mufindi Kaskazini ) na ukienda nyuma zaidi, 1995, sheria ya Jenerali Ulimwengu, CCM Taifa. Wabunge wanne tu kati ya mamia na mamia ya wabunge waliopata kuchaguliwa miaka 20, 30 iliyopita.
Aibu.
Pamoja na kuchagiza mjadala, je hiyo tafsiri ni rasmi? Je, unaweza kutupatia link ili nijiridhishe na tafsiri hiyo?