Jamani nasisitiza kwamba tusiwadanganye na kuwapotosha watu na wasomaji wetu wa JF hapa, ukweli ni kwamba kuhusu suala la Uhuru wa imani ya dini, suala hili lipo Ibara ya 41.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini
. Wakati Ibara ya 40 ya Katiba Inayopendekezwa kuhusu Uhuru wa habari na vyombo vya habari; (1) Kila mtu ana haki na uhuru wa: (a) kutafuta, kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa sahihi; na (b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari
."