mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Sheria ya kuwalinda Marais wastaafu, inawalinda na mafisadi wengine wengi.
Kwa mujibu wa katiba yetu, Rais wa Tanzania ana hadhi ya Mungu. Ni mtu ambaye anaweza kuelekeza wanasheria kinyume na sheria, madaktari kinyume na udaktari, Maengineer kinyume na u-engneer na bado hahojiwi. Rais wa Tanzania anaweza kusema hadharani mtu fulani afe, na akafa siku hiyo hiyo, na asichukuliwe hatua yeyote.
Ni mkataba gani wa kimataifa, utafanyika bila hisani ya mtu huyo mwenye nguvu kama hizo. Ni binadamu gani anaweza kufanya ufisadi mkubwa bila shiriki ya Rais? Hajipendi?
Sasa katika mazingira kama hayo, Je! Tunasubiri mafisadi washitakiwe?
Wakisema walitumwa na Rais, na huyo Rais hashitakiwi, tutawahukumu vipi?
Je! Si kweli kwamba mafisadi wanatumia mwanya huu wa sheria ya kinga ya Rais wakijua kuwa inawapa ulinzi na wao?
Ni kashfa ngapi nzito zimeibuliwa, na majina yametajwa bila kufikishwa mahakamani? Inahaitaji elimu ya uzamivu kujua kuwa sheria hii ya kinga ya Urais inawalinda na wengine?
All in all! Imani yangu kwa Rais yeyote atakayeona sawa kuongoza Tanzania kwa katiba iliyopo, ni imani batili.
Sent using Jamii Forums mobile app