Imani yangu kwa Tido Mhando

lukala

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
594
Reaction score
590
Habarini ndg, na samahanini pia sijui hii mada ningeiweka wapi kati ya jukwaa la michezo au la siasa.

Nirudi kwenye point, nimejaribu kufikiria hili jambo muda mrefu sana kwasasa nimeanza kupata majibu , hizi nchi zetu za Afrika tunakasumba mbaya sana kwa watu makini na weledi kama Ndg Mhando.

Huyu jamaa binafsi nimeanza kumskia BBC na kweli mambo yake pale yalikuwa hatari sana ,na fahamu alikuwa anafanya kazi na wazungu hakika jamaa aliwapiga bao sana wanzungu na kufanya bbc kwa huku kwetu kila ifikapo saa kumi na mbili watu wanapenda kuisikiliza taarifa zao.

Mwishoni mwa miaka ya 2000 kama sikosei huyu jamaa alirudi bongo kufanyia kazi rtd na Tvt duuu huyu jamaa ndiye aliyeibadilisha kutoka Tvt na kupelekea TBC. ..hakika ikawa kituo bora kabisa hapa Tz kwa kipindi kile lkn sijui kitu gani kilimtoa naamini figisu ambayo Waafrika siku zote hatutaki watu weredi.

Baada ya miaka kuanzia 2014 , huyu jamaa akaenda Azam media duu huyu jamaa hatarii Azam media licha ya uchanga wake huyu jamaa alianza ku- capture taratibu soko la Tz na East Africa kwa ujumla . Hii miaka minne tu tangu Azam media awepo pale leo hii ni kituo bora kabisa kwa East Afrika na central Africa and some part of South African zone.

Hivi najiuliza kama hawa TBC wangemuacha huyu jamaa na angetekeza majukumu yake kwa uhuru na kisayansi leo naamini Tbc ingeshika Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp kwani dokta ayubu rioba hatoshi?

Binafsi kutoka kwa dokta ayubu nilitegemea yafuatayo
1. TBC1 - HABARI ZA NDANI NA KIMATAIFA
2. TBC2 - MICHEZO
3. TBC3 - UTALII NA UTAMADUNI
4. TBC4 - SIASA NA MAENDELEO
5. TBC5 - TAMTHILIA NA SINEMA
6. TBC6 - MIZIKI

Anyway, ikimpendeza atafanya kabla hajaondoka.
 
Sio kwamba nampinga hapana , Bali mambo aliyofanya Tido akiwa mkurugenzi ni manzito kuliko huyu sijui tumpe muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule Azam yuko huru kufanya kazi yake! Huku TBC anasimamiwa na kina Pole pole na nilazima aunge mkono chama cha mapinduzi kuwahadaa wananchi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule Azam yuko huru kufanya kazi yake! Huku TBC anasimamiwa na kina Pole pole na nilazima aunge mkono chama cha mapinduzi kuwahadaa wananchi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa inaharibu sana professional za watu, hasa nchi za Afrika. Mimi naamini wapo wataalamu wengi sana lkn wapddo wengi sana akina Tido Mhando , hapa ndo namkumbuka Mh raisi alipozungumzia issue ya Mfugale kwenye Tanroads

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa tunakula fa ya uingereza ndani ya Azam TV jamaa anajitahidi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…