Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mara tangazo la raisi Bazoum kushikiliwa na walinzi wake lilipotoka ilionekana kama ni jaribio la mapinduzi ambalo lingeshindwa.Lakini hata hivyo kiongozi wa kikundi hicho Gen Abdourahmane Tchiani ambaye mwanzoni alitoa tangazo akiwa kifua wazi alionekana kukaza kamba na kuungwa mkono na kada nyengine za kijeshi.
Katika tangazo hilo kikundi hicho kilitoa onyo kwamba hakitaki uingiliaji kati wa mataifa ya nje.Kama kawaida mataifa hayo hayakuacha kutoa vitisho.Miongoni mwa mataifa yaliyotaka raisi Bazoum arudishwe madarakani haraka na jeshi lirudi kambini ni umoja wa ECOWAS.
Hatimae jana taifa la Marekani limetangaza kuondoa uungaji wake mkono kwa raisi Mohammed Bazoum na baadae umoja wa Ulaya nao umefuatia kusema unaondosha ushirikiano wake wote na taifa hilo pekee lililobaki kwa nchi za magharibi ya Afrika lililokuwa na ushirikiano nao baada ya mataifa mengine jirani kuamua kuachana na kupangiwa mambo yao na mataifa hayo hasa ufaransa iliyokuwa mkoloni wao.
Miongoni mwa sababu zilizotolewa na viongozi wapya wa mapinduzi ya Niger zilizowapelekea kuamua kumuondosha raisi Bazoum ni kudorora kwa hali ya uchumi na hasa usalama hata pamoja na kuwepo vikosi vya Ufaransa nchini humo na ambapo raisi Bazoum alikuwa mshirika wao mkubwa.
Vikosi vya kijeshi vya Ufaransa baada ya kutimuliwa kutoka nchi za Mali,Chad na Burkinafaso vilihamishia shughuli zake nchi humo na kwa Upande wa Marekani ina kituo chake kikubwa cha kuongoza droni za kupambana na wale inaowaita wapiganaji wa ISIS wenye mfungamano na Alqaeda chini ya tawi la Sahel.