Imefika Wakati Viwanda vya Sukari Viache Kulalamika!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Mwaka 2015 uwe ni mwaka wa mabadiliko kwa viwanda vya sukari nchini Tanzania. Sekta hii imekuwa 'baby seated' kwa kipindi kirefu na ninahofu huko mbeleni (hata sasa) haitawezekana kuendelea kuvilea kama ilivyokuwa kwenye viwanda vya cement, sasa serikali imeachia soko na tunaona simenti kutoka Pakstan n.k inaingia kwa wingi lakini bado viwanda vya ndani vinanawiri. Viwanda vya simenti kwa mfano vimewekeza sana kwenye masoko, kuunda distribution network pamoja na brand vya kutosha. Hata ije simenti ya Pakstani, lakini kama nafsini mwangu naikubali Twiga cement mathalani, nitainunua tu hata iwe bei juu.
Hivii, nani alishawahi ona Kilombero sugar au Kagera sugar waweweka tangazo lao kwenye TV kwa mfano ili kuvutia wateja wanunue brand yao? Viwanda vya sukari vimezoea kufanya biashara kwa mteremko, and am afraid now ni zamu yao kupanda milima. Waamke wawekeze kwenye masoko (marketing) 2015!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…