upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 119
- 144
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es salaam Edward Mpogoloe amesema kampeni ya ‘Hala Bi Mkubwa” iliyoanzishwa na Mtangazaji Barton Mwemba maarufu Mwijaku itasaidia kunadi kazi nzuri zilizofanywa chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika uzinduzi wa Kampeni hiyo, Edward Mpogolo amesema Rais Samia ameyafanya mambo mengi katika Nchi ikiwemo Wilaya ya Ilala ambako amepeleka zaidi ya shilingi bilioni mia tatu kwa ajili ya shughuli za maendeleo "pia kwenye eneo la elimu amefanya makubwa kuna shule za gorofa, nani anayeweza kuwaambia kwamba Mh. Rais amefanya hayo ? niwaombe Viongozi wenzangu huko Mwijaku anakokuja tumpe ushirikiano wa kutosha, tumpe data"