Imekaaje Rais kubadilishiwa msaidizi tena ugenini?

Imekaaje Rais kubadilishiwa msaidizi tena ugenini?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Inafahamika kuwa Marais huwa na wasaidizi wao, kwa hapa kwetu msaidizi wa Rais ndio huwa karibu na Rais na huteuliwa kwa uyakinifu.

Nini hiki kinachotokea Kenya kuona Rais wetu anamsaidizi mwengine tena nahisi si kutoka katika taifa letu. Kiusalama ni nini hii?

Je, ulinzi wa Rais wetu upo kiumakini kweli au ni kawaida?

Ni Utaratibu Wa Kawaida Pia Upo Tangu Kitambo Sana
Siyo Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Huyu Bali Wote
 
Ni Utaratibu Wa Kawaida Pia Upo Tangu Kitambo Sana
Siyo Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Huyu Bali Wote
Mambo ya kawaida,wajameni nyie hata hamkusikia blass band wakiimba "Tazama ramani"
"Nakupenda TZ"
Mama alipewa nafasi ya kuchagua hizo nyimbo,kwa wiki nzima kikosi Cha blass band Cha KDF kilikuwa kinafanya Mazoezi.
Na kuhusu usalama,hivi mnafikiri hata kama mngepereka makomandoo wote wa JWTZ,Wamlinde,ndio angekuwa salama?!
Kuna Raisi wa US aliuliwa na risasi akiwa kwenye ziara ndani ya US Tena chini ya ulinzi mkali
 
1620357854399.png

KENZY,

..unamuona Rais Chakwera wa Mlw alipotembelea Tz alipewa MPAMBE toka Jwtz?

..kilichotokea kwa Mama Samia alipokwenda Kny na kupewa mpambe toka Kdf ni jambo la kawaida.
 
Inafahamika kuwa Marais huwa na wasaidizi wao, kwa hapa kwetu msaidizi wa Rais ndio huwa karibu na Rais na huteuliwa kwa uyakinifu.

Nini hiki kinachotokea Kenya kuona Rais wetu anamsaidizi mwengine tena nahisi si kutoka katika taifa letu. Kiusalama ni nini hii?

Je, ulinzi wa Rais wetu upo kiumakini kweli au ni kawaida?

Kama msaidizi tuliyemzoea anaumwa?
 
Hii nchi ina vichaa wengi sana wanaojifanya wajuaji.
Juzi mmoja kaja hapa eeehh inakuwaje Rais wetu apokelewe na Waziri wa mambo ya nje!!!!
Hata kukujibu naona kazi ila shortly fahamu kuwa watu wanajua kuliko wewe unayejifanya unajua kisa kijiweni kwako wanakuona kichwa.
 
Back
Top Bottom