Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Mkubwa usiiache ipite
Tuma barua kwa waziri, director wa hospital service, mganga mkuu wa Mount Meru na RMO lakini pia hakikisha unapata mwanasheria mzuri

Pole sana lakini hii ndio hali halisi ya Tanzania kwa sasa... kila mtu kwenye idara karibia zote ni rais, waziri, mbunge, afisa utawala na spika... wachache sana wameamua kuendelea kujitolea

Kibaya zaidi ni kwamba tunamalizia hasira zetu kwa ndugu zetu wapendwa na kuacha wahusika wa chuki zetu wakiwa wamelalia vyumba vya mamia ya mamilioni ya pesa

Nadhani Dr. Longdare anafahamika na kuna watu walio karibu nae, hakikisha anapata hizi complaints katika family level na pia offcially

USIACHE LIPITE KWANI HAKI HAIPOTEI IWE NZURI AU MBAYA, UKIIACHA IPOTEE, ROHO YA MALAIKA DORRIS ITAKUSUTA
 
pole sana tumepoteza mjukuu kizembe nchi hii kwa sasa kila sekta imeharibika wanakula pesa na wanatoa huduma feki mungu amlaze mahala pema peponi mjukuu
 
madaktari na manerse wa leo hawana wito wa kazi zao kabisa, pole sana kwa yaliokukuta mkuu
 
mkuu nitapingana na hatua yoyote unayotaka kuwachukulia hawa watu zaidi tu ya kwenda kuwashauri.kwa sababu i hope wapo wachache pale so mkiwafukuza huduma haitakuwepo tena , but kawa madokta wapo wengi ,ok hamna shida
Acha utoto wewe, Kwa vile wapo wachache waendelee na kuwaua wagonjwa na sote tukae pembeni tukiwashangilia? Mbona huna huruma hivi? Nimesoma majibu ya wana JF bado sijapata lililonikuna. Mimi naamini anachotitaji mwasilisha mada ni ushauri wa nini kifanyike au afanye ili upuuzi huu usirudiwe tena. Naamini humu ndani wapo wenzetu waliobobea katika fani ya sheria wanaoweza kutufungua macho.
Uoza wa namna hii upo karibu katika kila pembe ya nchi. Ni lazima hatua za kuukomesha zianze sasa. Tutafakari,Tuchukue hatua kama Great Thinkers.
 
POLENI SANA blue balaa na family yako........INASIKITISHA mazingira ya kifo cha mjukuu wako kimetokana na uzembe wa ma DR na manesi wa hosp zote ulizopitia....japo tunajua kifo ni lazima kwa kila Bin Adam lakin huduma mbovu zinachangia vifo vya kizembe. Hao wakichuliwa hatua za kinidhamu itasaidia kuzuia vifo vya kizembe kwa wagonjwa wengine. Huyo aliyesema u PM na kumpa detail nyingne nyingi mpe anaweza kutoa msaada wa kuwa adabisha hao ma DR na manesi wengine....POLE SANA, BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.......
 
Mkuu Pole sana, nimeumia sana tena sana inanikumbusha kifo cha mama yangu wakati niko mdogo sana, alifariki eti kwa kukosa maji(drips) maana aliharisha na kutapika sana, kutokana na umasikini wa familia yangu manesi wakakataa kutoa huduma wakitaka hongo....RIP Dorris...
 

Asante sana na pole wewe pia
 

Asante sana pole na wewe pia
 

Asante na nimesha anza move
 

Thanks and will PM you shortly
 
Yaani nimebahatika kusoma kisa hiki cha kusikitisha baada ya Ku google "Eben Hospital Arusha" ambapo kuna ndugu yangu kaniambia kuwa ameenda huko kufanyowa dabo cheki baada ya kutibiwa St Thomas na hali kuendelea kuwa mbaya. Sasa ndo nikapata mshtuko wa habari hii.

BLUE BALAA bado upo humu?
 
Mkuu, Umeshapata Mjukuu Mwingine, Au!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…