Imeniuma sana

Sijasoma maoni ya wadau wengine ila nimesoma kwa makini mada husika, hakika huu ni unyama mbaya sana kwenye ndoa lakini sintosita kumwita mwanume huyo kuwa ni hayawani na mzandiki wa kutupwa hasiyefaaa kukaa katika jamii ya watu na hata ya wanyama kwani nao wana mfumo wao wa maisha. Mpe pole sana huyo sasa mwambie MUNGU ni mwema na atamlinda siku zote za maisha yake.
 
Babra mpendwa, pole sana kwa yaliyomsibu rafiki yako mpenzi. Kusema kweli wanaume wanaopiga maGF wao au wake zao mimi wananikera sana. Kwa sababu sioni sababu yoyote ile inayohalalisha mwanaume kumpiga GF wake au Mkewe. Kama unamuona mmeshindana basi chukua 50 zako lakini siyo kumpiga na kutaka kumtia ukilema au hata kumuua.

Sasa kama huyu dada maskini ya Mungu hakuwa na kosa lolote lililostahili kumsababishia kipigo kiasi hiki hadi kuharibu mimba yake. Alichofanya kwa kuuliza ujumbe aliouona kwenye simu ya mume wake ni haki yake na ni haki ya mwanandoa yoyote yule awe mwanaume au mwanamke pindi akikutana na ujumbe kama huo katika simu ya mkewe/mumewe. Sasa kipigo kama hiki kwa kuuliza tu kulikoni na ujumbe aliouna. Je, kama huyu binti angekuwa ametenda kosa si ndiyo angemuua kabisa!

Kwa wanawake ambao bado hamjaolewa lakini mna maBF wenye tabia ya kuwapiga, lazima muwe na msimamo thabiti ili kuzuia na kukomesha kabisa hali hii ya unyanyasaji wa hali ya juu inayofanywa na baadhi ya wanaume dhidi yenu.

Babra nakuomba utuhabarishe rafikiyo anavyoendelea na matibabu…. GOD FORBID kama hali yake itabadilika na mabaya zaidi kutokea kitu ambacho hatuombei, basi huyu jamaa ni lazima mumfikishe kwenye sheria bila kumuogopa wala kumuonea haya.
 
Babra, I'm deeply sorry for your friend's situation..

Hata kama aligusa simu ya mumewe, hakika hakustahili kufanyia alivyofanyiwa..Yaani badala ya wanandoa kuwa pia marafiki kwenye ndoa ni uadui,hasira na jazba vimetawala..Mwisho wa siku unabaki kumwogopa tu mtu huku upendo umechuja!

Ndo mana nikisikia mtu kadivorce naheshimu sana maamuzi yake mana sijui nini kimempelekea kufanya hivyo,watu wanapitia mengi..Uvumilivu una kikomo!

Uguza pole mamii Babra!..
 
Am speechless. Pole sana Babra.
To wise men like you Nguli na mimi Sipo na wengineo hili ni tukio baya sana kumfanyia mwanamke sembuse mkeo unayempenda kwa dhati
 
To wise men like you Nguli na mimi Sipo na wengineo hili ni tukio baya sana kumfanyia mwanamke sembuse mkeo unayempenda kwa dhati
Well said..siamini katka mapenzi ya ukatili huu kwamba mwanamke hana haki ya kuhoji?? Then ni kukaa pamoja au wawili wapendanao?? And iam so dissapointed kwa wale wanaofikiri kuzuia kugusa simu ya mwenzio ndo solution ya ndoa??? Kuhalalisha kucheat?? Au nidhamu ya kijinga hii??
And some proudly wanaropoka marufuku my wf kugusa simu yangu???omw...
 
Kwenye hizo sehemu nilizohighlight ni sehemu ambazo tusipokuwa makini hakika mahusiano yetu yatakuwa magumu siku zote. hili ni tukio baya sana kwa wanaume na linatudhalilisha sana
 
Its really hard to understand certain men, how on earth can you beat a woman and above all A PREGNANT WOMAN? Is he that crazy not to care for the life his wife was carrying in her womb? I know you might all disagree with me but I think Babra's friend should leave her husband kabisa, he doesnt deserve a woman like her.
 
nadhani yuko nje ya mpango wa Mungu, maana Mungu ameagiza mwanamke kuwa msaidizi wa mwanaume kwa mambo ya kijamii na si wa kumpiga, huyu anahitaji elimu, Mwanamke ni utukufu kwa mwanaume na kama vile Kristo alivyo kiongozi wa wote....
 
Babra,pole sana kwa masahibu yaliyomkuta rafiki yako.Binafsi nimesikitika na kuumia sana kwa ukatili huu alioufanya huyu Msukuma Chipolopolo(sidhani kama ni Msukuma wa ukweli huyu maana wasukuma hatuna tabia kama hizi alizozionesha huyu bwana)..Kwa kweli inauma sana

-Kwanza amekuwa akimcheat mkewe(hii ni tabia mbaya kabisa kwa sisi wasukuma) hili ni kosa kubwa

-Pili mkewe kafuma sms jamaa aulizwa aanza kumpiga mkewe na hatimaye mama anapoteza ujauzito wake na kuumia vibaya kiasi cha kupoteza fahamu,hili nalo ni kosa kubwa mnoooo hasa kwa watu waliopendana na hatimaye kufunga ndoa(wasukuma hatuko hivi kabisa,wasukuma tunamthamini haswa mwanamke,huyu jamaa yawezekana ni chipolopolo kama alivyosema Geof ama yawezekana ni ulimbukeni ama ni mambo ya ndogo(TiGo) toka kwa nyumba ndogo ndo yamemchanganya kiasi cha kumfanya mkewe wa ndoa asiwe na thamani machoni mwake)..Jamaa kaharibu kwa kweli

-Tatu jamaa kachemka zaidi kwa kutokomea kusikojulikana baada ya kumdunda mkewe na hatimaye kupelekea miscarriage kwa huyo mama..Yaani kweli mkeo wa ndoa unampiga mpaka anazirai halafu unaingia mitini bila kuchukua hatua yoyote kuyanusuru naisha yake!!!!!mhapana wasukuma hatupo hivi bana(limbwata???)...Inasikitisha kweli

Babra,baada ya masahibu yote haya kuna hatua zote za kisheria(kuripoti polisi n.k) zimefanyika ili kumuadabisha Mwanahizaya huyu???,nadhani uko Moshi sasa,mgonjwa anaendeleaje?,mpe pole sana.....Any news kuhusu whereabouts za huyo bwana?
 
Halafu Babra,hao ndugu wana muda gani katika ndoa yao???,wana watoto??..Kama vp ni heri aachane na huyo jamaa(talaka) maana kinachoonekana so far ni kwamba mapenzi ya jamaa kwa mkewe tayari yameexpire so ni bora rafikiyo akachukua tu ustaarabu wake maana inakoelekea jamaa anaweza kuja kumuua siku moja(kama amaediriki kuondoka na kwenda kuskojulikana ilhali mkewe yu mgonjwa mahututi kazirai na mimba imeharibika ni dhahiri kwamba mapenzi ya huyu bwana kwa mkewe yamekwisha)

NB
Nadhani hili pia ni fundisho kwa wanandoa/wapenzi katika suala zima la privacy kwenye mambo ya mobile phones na barua pepe(e mails),tuwe waangalifu kwa kweli na ni bora tukaheshimu privacy za wenza wetu...Pia daima tuwe waaminifu katika ndoa zetu/mahusiano yetu
 

Homeboy, vipi mbona umeingia mzima mzima na ushauri wa Beijing? Umeweka contigency plans za kumsaidia akiondoka kwenye hiyo ndoa?

Jamani domestic violence zipo kila mara katika jamii zetu. Tuache kutoa huu ushauri wa kuachana. It doesnt help at all. Cha kufanya ni kumuwajibisha huyu baba. Kama ana kosa ashikishwe adabu. Otherwise kila kukicha mkitoa ushauri wa ndoa kuisha..nadhani tuna-condone haya mambo. Talaka zitatolewa ngapi?

Let the guy be punished. Kumbukeni kuna watoto ambao wanahitaji malezi. Tuache ideas za watu kuachana. Bali tukemee hizi tabia mbovu.
 
Babra, I am very sorry for your dear friend.
That wife beater needs to face the full extent of the law.
In this day and age he can beat his pregnant wife till she miscarries? I imagine then that he had no love for her right from the beginning.
tumuombe Mungu, apone haraka sana.
God Bless you for your effort.
 
Babra poleni sana kwa tukio hili na ni maombi yangu kwamba Mungu amponye mama huyo.

Suala la ndoa/familia linahitaji uponyaji wa KiMungu; kama ndoa haijaingia dosari yoyote sioni shida ya mke/mme kutumia simu ya mwenzake. Mwanaume unapomkataza mke wako kusoma message zilizoko kwenye simu yako au kupokea simu yako kama mtu amepiga maana yake unalo jambo unaloficha. Na hapa ndipo kwenye tatizo ambako tunapaswa kutibu.

Kitu kingine kinachonipa shida ni utamaduni ambao jamii imejiwekea kuwa mvulana/mwanaume kutembea na wasichana/wanawake wengine ni kama jambo linalotaka kuhalalishwa na kuwa la kawaida na hivyo mwanaume anaona kama ni haki yake kuwa na nyumba ndogo. Msichana/mwanamke akidiriki kufanya hivyo anaitwa Malaya lakini mwanaume siyo!!!!!!

Nimefika mahali nawaza kwamba wachungaji pamoja na kuwahubiri watu wamjue Mungu lakini nafikiri ipo haja ya kuanzisha huduma ya kuwasaidia vijana wa kike na kiume wasiwe na mahusiano (kumegana/kumega/kumegwa) kabla ya ndoa huenda ikawasidia wanaume baada ya kuoa wakaridhika/kutosheka na wake zao.

Yako mambo mawili ambayo yamenisaidia kufurahia ndoa yangu;

1. Nikiwa kijana nilisema na kuazimia moyoni kuwa sitafanya mahusiano yoyote na msichana/mwanamke yatakayofikia hatua ya kumegana kwani sitaki aje awepo yeyote atakayejidai kuwa alinijua kabla ya mke wangu na kupelekea yeye kumdharau mke wangu.

2. Pili mimi mwenyewe nilisema nisije nikawa na msichana/mwanamke mwingine ambaye nitakuwa nalinganisha mapenzi aliyokuwa ananipa na anayonipa mke wangu. Hii imenisaidia kwani what I get is the best as I don't have a comparison.

Kumbuka suala la uzinzi/uasherati halitegemei dini/dhehebu lako ni suala la nidhamu unayoweka katika jambo hili. Ridhika na mke/mme wako na kamwe usiendekeze mahusiano ya karibu na jinsia tofauti lazima utaingia kwenye mtego. Epuka kumuingiza mtu majaribuni au kujiingiza majaribuni katika jambo hili, kwa kufanya hivi utaiponya nafsi yako, utamponya mme/mke wako na utawaponya watoto wako.
 
Na ikiwa fiction, utakuwa umetuibia mawazo yetu Babra!.


How come mwanaume timamu ukamrukia mkewe wa ndoa (tena mja mzito) kwa sababu ameshika simu yako na kukuta jina "han" tu?...nahitaji details zaidi ili kuchangia, may b upande wa pili haujapewa fursa zaidi wa kusikilizwa. Babra, mleta stori hii amejieleza kuwa yeye ni rafiki kipenzi wa wa mwathirika (mwanamke wenzie).


Babra anasema yeye ameelezwa tu kwa hiyo hajui undani zaidi ya yale aliyoelezwa, hapaswa kutoa hukumu wala kujenga hoja kuwa huyo mwanaume hafai kabisa kabsa hajafika hapo kwenye eneo la tukio na kujua undani wa haya.


Be Careful Babra!.
 
Babra, kama ni utani, dont do it! Is this true and happerning at this age?

mambo gani haya?
 


haya yamenikuta pia japo mimi sikutake action yeyote,nilmuacha tu mtu(mchumba)nilikuta kasave jina langu tofauti(weekend)nikahis ana multple lovers
 

Ni kweli bro tuwe makini lakini kitendo cha mwanaume kunyanyua mkono na kumpiga mkewe mjamzito hadi apate miscarrage? Hata kama hilo kosa ni kubwa kiasi gani angefanya uamuzi wa kumfukuza arudi kwao but kipio cha mbwa mwizi hapana!! Unless amethibitisha kuwa mimba hiyo si yake na mke amemcheat- kitu ambacho hata kama ni hicho kumpiga its a big no- watu hawaogopi murder case siku hizi eeh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…