Imeshawahi kukutokea?

cacutee

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2024
Posts
1,333
Reaction score
3,512
Wapendwa heri ya nwaka mpya 2025. Binafsi ninaamini kulingana na maandiko matakatifu katika kitabu cha mwanzo kwenye ile sura inayozungumzia uumbaji siku inaanza jioni (' ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya..... '). Hivyo Mimi nimeshauona mwaka mpya 2025.

Baada ya salamu za mwaka mpya ninaomba kuwauliza wananchi wenzangu wa Tanzania kama imeshawahi kukutokea umekutana na mtu online hujawahi kuonana nae... Mkawasiliana kwa mda mrefu kiasi kwamba kila mmoja mbali na kwamba hajawahi kuonana na mwenzake lakini ameshakuwa sehemu ya mwingine? Kwamba kama ikitokea hajawasiliana na wewe unaumia? Halafu gafla huyu mtu akapotea na hujawahi wasiliana nae tena?
Katika harakati za hapa na pale katika mtandao fulani ww kijamii mbali nanJF nimekutana na huyu bwana Derick (sio jina lake). Alini text tu kuuliza kitu flani tukajikuta tunawasiliana kwa mda mrefu kiasi kwamba nilihisi kama nimeshawahi kumuona uso kwa uso.
Ghafla bwana huyu amekuwa kimya na amepotea hewani. Kwakweli nimejikuta ninaumia Ila nikajiona mjinga kwanini niumie kwa mtu ambaye sikuwahi kumuona live? Yani ile week mood yangu iliharibika kwakweli.
Sasa bwana Derick popote ulipo kama utapita hapa maana najua uko JF ninaomba ujue kwamba kutoweka kwako ghafla hakujanifurahisha (wamakonde wanasema 'hakujaninogea bwana wewee')
Ni hayo tu ndugu zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…