Elections 2015 Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Baada ya Mwanakijiji kuchagua upande wa shetani, minakasha nyeti kama hii hatii maguu.

Mwanangu kua uyaone......
 
Uko sahihi mkuu. Ni ubabe tu. Sadifa aliwahi sema kuwa CCM wana mbinu zaidi ya MUNGU. That means mbinu za kishetani.
 
tic....tic....tic....
 
PASCO
Usisahau kuwa EL alipatakura nyingi pia kutokana na mashabiki wake ndani ya ccm hivyo kwa kuzitumia takwimu hizo bila kutohoa za mashabiki hao, huwezi pata kura halisi
 
Ubishi hauwezi kwisha ikiwa bashite asema yeye hajazaliwa kolomije na yeye ndie Paul Christian Makonda wa ukweli basi nayende yendavyo .
Lakini IPO siku isojina
 
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
  1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
  2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
  3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
  4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
  5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
  6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
  7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
  8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
  9. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
  10. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  11. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
  12. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Paschal katika bora wako enzi hizo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…