Sumbi Sanchez
Senior Member
- Apr 16, 2017
- 100
- 355
IMEWEZEKANAJE BILA CLOUDS FM?
Kuna nyimbo nyingi mno miaka ya karibuni ambazo ni maarufu kupita kiasi ingawa hazikuwahi kupewa airtime na Clouds FM. Inashangaza mno. Hivi wimbo unawezaje kuwa maarufu bila kusikika kwenye Mawingu FM. Wimbo unawezaje kujulikana kila mahali bila kusifiwa na B Dozen au Adam Mchomvu ambao ndio wataalamu wa kuzitambua nyimbo kali na mbovu. Ndio wanaoamua msanii yupi awe juu ya wengine.
Lakini ngoma zifuatazo zina umaarufu wa kushangaza wakati Dozen na vijana wake wa XXL hawajawahi kuzibariki. Hebu jionee orodha.
1) Kwangwaru (Harmonize ft Diamond) - 54M views On YouTube
2) Tetema (Rayvanny ft Diamond) - 32M views on YouTube
3) Inama (Diamond)
4) Nadekezwa (Mbosso)
5) Katika (Navy Kenzo ft Diamond Platnumz)
6) Bora tuachane (Lavalava)
7) Ndindindi (Jay Dee)
8) Hodari (Mbosso)
9) Jibebe (Diamond, Lavalava na Mboso)
10) Yahaya (Jay Dee)
Anyway hizo views za YouTube tusizingatie sana maana Diamond na WCB wote huwa wananunua views. Na hata namna zinavyohit huku mtaani sio bure. Nina mashaka huenda Diamond na timu yake huwa wanatoa hongo kwa wale wenye vibanda vya library za kuingizia nyimbo huku mtaani ili wazipe promo nyimbo zao. Huenda na maDJ wa klabu pia watakuwa wananunuliwa na hawa jamaa.
Hata wazi kuwa mambo si kama yalivyokuwa kwa CMG. Msanii anaweza kutikisa kupita kiasi hata bila sapoti yao. Hakuna nyimbo ya Mbosso (kama solo artist) imewahi kupigwa Mawingu FM. Lakini hapana shaka Mbosso ni kati ya wanamuziki wanaosumbua mno kwa sasa nchini Tanzania na Afrika Mashariki.
Kosa la CMG lilikuwa kuamua kumkweza Diamond juu zaidi ya wengine halafu eti bado wakataka wamtawale wanavyotaka wao kama wanavyowafanya wasanii wengine. Wasanii sasa hawana hofu tena ya kuzimiwa data na Mawingu FM. Huu ni ushindi kwa wasanii wote.
Hata huyu Harmonize ambaye kwa sasa wanamuunga mkono hana hofu yoyote wala sababu ya kuwaogopa kwa kuwa amekuwa juu bila sapoti yao na ana uwezo wa kuendelea kuwa juu bila wao. Wamkweze kuliko wasanii wengine kwa kuamini kuwa kutaitikisa nguvu ya Diamond lakini wakumbuke hawana uwezo wa kumtawala wanavyotaka wao maana sanaa imezaliwa upya.