Imewezekaje bila Clouds FM?

Sumbi Sanchez

Senior Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
100
Reaction score
355
IMEWEZEKANAJE BILA CLOUDS FM?

Kuna nyimbo nyingi mno miaka ya karibuni ambazo ni maarufu kupita kiasi ingawa hazikuwahi kupewa airtime na Clouds FM. Inashangaza mno. Hivi wimbo unawezaje kuwa maarufu bila kusikika kwenye Mawingu FM. Wimbo unawezaje kujulikana kila mahali bila kusifiwa na B Dozen au Adam Mchomvu ambao ndio wataalamu wa kuzitambua nyimbo kali na mbovu. Ndio wanaoamua msanii yupi awe juu ya wengine.

Lakini ngoma zifuatazo zina umaarufu wa kushangaza wakati Dozen na vijana wake wa XXL hawajawahi kuzibariki. Hebu jionee orodha.

1) Kwangwaru (Harmonize ft Diamond) - 54M views On YouTube

2) Tetema (Rayvanny ft Diamond) - 32M views on YouTube

3) Inama (Diamond)

4) Nadekezwa (Mbosso)

5) Katika (Navy Kenzo ft Diamond Platnumz)

6) Bora tuachane (Lavalava)

7) Ndindindi (Jay Dee)

8) Hodari (Mbosso)

9) Jibebe (Diamond, Lavalava na Mboso)

10) Yahaya (Jay Dee)


Anyway hizo views za YouTube tusizingatie sana maana Diamond na WCB wote huwa wananunua views. Na hata namna zinavyohit huku mtaani sio bure. Nina mashaka huenda Diamond na timu yake huwa wanatoa hongo kwa wale wenye vibanda vya library za kuingizia nyimbo huku mtaani ili wazipe promo nyimbo zao. Huenda na maDJ wa klabu pia watakuwa wananunuliwa na hawa jamaa.

Hata wazi kuwa mambo si kama yalivyokuwa kwa CMG. Msanii anaweza kutikisa kupita kiasi hata bila sapoti yao. Hakuna nyimbo ya Mbosso (kama solo artist) imewahi kupigwa Mawingu FM. Lakini hapana shaka Mbosso ni kati ya wanamuziki wanaosumbua mno kwa sasa nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Kosa la CMG lilikuwa kuamua kumkweza Diamond juu zaidi ya wengine halafu eti bado wakataka wamtawale wanavyotaka wao kama wanavyowafanya wasanii wengine. Wasanii sasa hawana hofu tena ya kuzimiwa data na Mawingu FM. Huu ni ushindi kwa wasanii wote.

Hata huyu Harmonize ambaye kwa sasa wanamuunga mkono hana hofu yoyote wala sababu ya kuwaogopa kwa kuwa amekuwa juu bila sapoti yao na ana uwezo wa kuendelea kuwa juu bila wao. Wamkweze kuliko wasanii wengine kwa kuamini kuwa kutaitikisa nguvu ya Diamond lakini wakumbuke hawana uwezo wa kumtawala wanavyotaka wao maana sanaa imezaliwa upya.
 
Mbona Alikiba ni mkubwa kisanii kuliko Diamond.. Ana tuzo adi za BET, MTV nk .. Ameimba na wasanii wakubwa kama Chriss brown, Jason derulo, Drake, Future, Migos.... Na yote kwasababu clouds wanampa promo




Sitaki maswali kuhusu hizo tuzo na collaboration maana alikiba sio mtu wa kujionyesha

YOOO
 
Kitu kizuri ni kizuri tu hata ukiziwie kitajiuza yu chenyewe bila promotions. Wimbo wa banjuka juu wa DNA ulikaa mwakaa mzima umetoka ila haupo hit.. after a while ilikuja kua bonge la ngoma East Afrika.

Yaani ndio ile unafunga mlango unakuta mpo ndani nao..unazima muziki shabiki wanabak kwa dancefloor
 
@umbi Sanchez,Umeongea vizuri ila hao wasanii wote Hakuna aliyetoka au kujulikana kwa jamii bila kupitia clouds hata huyu marioo ni clouds ndo wanampa nafasi pinga kwa hoja sio ushabiki
 
Hiyo listi pc kubwa ni ya WCB ambayo tunajua nguvu yao,,huyo mbosso unadhani bila kwenda WCB angekuwa hapo alipo??..taja wengine

Point unayotakiwa kuisema ni kuwa ni rahisi sana msanii kuwa juu akijiunga na WCB kwani wana fans wengi ambao wanapenda chochote hata kibaya kutoka wasafi..
 
Kweli makonda baba yenu!..eti huu nao uzi?! mji wote umezizima giza totoro ni "mshumaa" mmoja 2 unaowaka...ww bdo unawawaza wasio na malinda?!.. akili mbovu kbsa izi km za babaenu bashite!
 
Diamond ni msanii ambaye kakuzwa na clouds ila yeye kidogo alikuwa na njaa ya kufika mbali tofaut na wasanii wengne, ndo mana alijifunza njia zote kipindi yuko na ukaribu na Ruge,So pia hao wasanii wote ulio wataja mafanikio yao mpaka kufika hapo nguvu ya clouds ipo,ila kama huna jicho la kutambua mambo huwez kujua hilo,Kila chenye mwanzo kina mwisho ila ni vema kuipa clouds heshima pale unapo sifia mafanikio ya Diamond.
 
Ukweli mchungu washaanza kupoteza ushawishi,kutoka mikoa 15 mpaka mikoa 7 kutoka elfu 10 mpaka elfu 5,shida yao moja tu beef la mtu mmoja wanalifanya linakuwa la taasisi.

Dunia imebadilika,mabadiliko ya kidigital yamesababisha platforms za kusambaza na kupromote mziki ziwe nyingi,sio kama zamani wakisema hutoki jua hutoki kweli.
 
Hapo Wimbo ni Kwangwalu tu, hayo Mengine ni Matakataka
 
kuna huyu jamaa anaitwa Badest47 mzee wa nikagongee promo ameipata baadae nyimbo ikiwa ishasumbua mpaka basi Wakaona isiwe mbaya wamsogeze mjengoni
 
 
rogger dat
 
Hiyo ngoma Clouds ndo wameileta mjini..Hata yeye mwenyewe amekiri hilo..kaangalie interview aliyofanya na XXL..Hiyo ngoma ilikuwa kubwa huko Mbeya na sio Tanzania nzima
Bardest 47 mzee wa nikagongee
 
kuna huyu jamaa anaitwa Badest47 mzee wa nikagongee promo ameipata baadae nyimbo ikiwa ishasumbua mpaka basi Wakaona isiwe mbaya wamsogeze mjengoni
Yes wakati Niko mbeya huo ndio ulikuwa wimbo wao wa taifa,pili kwenye huu muziki bila kuonana na wadau wa muziki wenye muziki wao huwezi kutoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…