Elections 2010 Imf yaionya serikali ya tanzania

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2010
Posts
375
Reaction score
195
Shirika la fedha la kimataifa (IMF) limesema matumizi ya serikali ya Tanzania yamekuwa yakiongezeka kwenye mambo ambayo sio maendeleo ya kama vile kulipa mishahara.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa IMF nchini Bw John Wakeman Linn amesema kuanzia mwaka 2007/2008 mapato ya ndani yalipungua kutoka 17% ya pato la taifa hadi chini ya 15% mwaka 2009/2010.
Wakati pato la taifa likipungua, hali inaonyesha matumizi ya serikali yakliongezeka mwaka 2007/2008 toka 18% hadi 28% ya pato la taifa mwaka 2009/2010.
Pia alisema tanzania imeendelea kukopa ZAIDI ili kugharamia matumizi haya ya uendeshaji!

MY TAKE: Je, watanzania mnataka kuambiwa mara ngapi kuwa CCM inakoipeleka nchi ni kubaya? Matumizi ya kiuendeshaji yanaongezeka,serikali inakopa zaidi kugharimia matumizi ya uendeshaji, BADO wazee wastaafu wa Afrika Mashariki hawalipwi, waalimu na waajiriwa wengi wa umma hawalipwi malimbikizo yao;
:thinking:TUJIULIZE: Hizi fedha zinakwenda wapi,nani analipwa hii mishahara minono? Na je serikali inasemaje kuhusu hili!:thinking:
Wana JF, naomba kuwakilisha.......

Source, Mwananchi Alhamis Octoba 28 2010, ukarasa wa tano
 
'kuichagua ccm tena itakuwa ni maafa ' - dr. slaa
 
penye wekundu pananisikitisha kweli duuuuuu!
 
Cha ajabu watumishi wa umma hawazidi 500,000 (stand to be corrected)
 

Bado siku 3 za kupima akili kwa wanaopanga kukipigia kura Chama Cha Mafisadi (CCM)
 
Wangekuwa wanakopa kuendeleza nchi ingekuwa afadhali. Wanakopa na kugawana kifamilia. Rubbish!
 

Dawa ya hii serikali ya kifisadi ni kuifukuza Ikulu na Bungeni mara moja ili tuanze kujipanga upya vinginevyo tuna laana ya umasikini tu................
 
'kuichagua ccm tena itakuwa ni maafa ' - dr. slaa

Maafa ya kutisha.

1. Bei zitaongezeka mara dufu kurudisha fedha walizochukua kwa wafanya biashara
2.Familia ya Kikwete itajilipa baada ya kutoswa na wakuu wa CCM na kujifanyia kampeni wenyewe.
3.Mkwere atalipiza kisasi kwa wale wote waliomatosa kipindi cha kampeni.
4.Hatajali kufuja mali kwa sababu muda hatagombea tena 2015
5. Nch itaendeshwa kibabe babe na familia ya Kikwete
6. N.K
 

6. Mikopo kwa elimu ya juu haitatolewa kwa sababu pesa zote zimeishia kwenye uchaguzi
7.
[/LIST]
[/LIST]

[/LIST]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…