Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Uamuzi wa Heche wa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA unaweza kukisaidia sana chama chake kwa sababu zifuatazo:
1. Hotuba yake imeonekana level heade. Kuingia kwa Heche katika kinyang'anyiro hiki kinafungua milango kwa kuwapa watu option ya kuwapigia kura Mbowe na Heche. Hii ina faida zijayo:
1. Hawatampoteza Mbowe ambae bado watu wengine wanaamini bado anahitajika sana.
2. Kuchaguliwa kwa Heche kutaipa kambi ya Lissu imani kuwa yuko mtu ambae atawasha moto chini ya Mbowe na kukifanya chama kiwe radical zaidi.
3. Sidhani kama Lissu anautaka sana uenyekiti wa CDM. Alifanya uamuzi wa haraka alipoamini kuwa Mbowe anamtumia Wenje kumtoa katika uongozi. Akishindwa, bado atakuwa na nafasi nzuri kugombea mwaka 2030 ambapo bila shaka Mbowe atawajibika kumuunga mkono.
4. Lissu akishindwa atakuwa huru ku focus kwenye uchaguzi wa urais wa JMT ambao ndio hasa anautaka.
5. Kwa vyovyote vile Lissu atakuwa mjumbe wa Kamati Kuu na hivyo ataweza kuisukumiza ajenda zake. Na ataweza kutumia wakati huo kusahihisha madhaifu ya kiongozi ambayo ameshutumiwa kuwa nayo.
6. Mbowe na Lissu watapata heshima kubwa kwa kuzuia mpasuko ambao washindani wao wangeufurahia. Lissu akijitoa na kusema kuwa anafanya hivyo ili kuzuia mpasuko ndani ya chama atapata heshima zaidi na shukrani za dhati za Mwenyekiti wake. Hii itampa nguvu zaidi ndani ya chama. Watu wa Clubhouse watakasirika lakini hawatakuwa na lakufanya.
7. Wenje ataendelea kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na kuweka balance dhidi ya radicals.
Wakifanya hivi, CDM itatoka katika mtifuano huu ikiwa imeimarika zaidi na kujiweka katika nafasi nzuri kwa uchaguzi wa mwaka huu.
Amandla...