Rchingalo,
Kwa uzoefu wangu mdogo nilio nao kwenye importation ya magari, ukitaka kukwepa kulipa uchakavu hakikisha gari unalo-import lisiwe chini ya mwaka 2000. Mwongozo uliotolewa na kupitishwa na bunge ni kwamba gari likizidi miaka kumi basi linapashwa kulipiwa uchakavu lakini wenzetu wa TRA kwa kuwa wao wanaangalia na kuzingatia kuvuka malengo ya kukusanya ushuru (hawaangalii hizo pesa wanazokusanya zinatumika vipi), basi wameamua kwa makusudi kupindisha rasimu iliyopitishwa na bunge. Katika mazingira ya kawaida, gari la mwaka 1999 ndio kwanza limefikisha miaka kumi hivyo alipashwi kulipiwa uchakavu. Lakini TRA amini usiamini ukilileta mwaka huu watakutoza ushuru wa uchakavu.
Labda mwana JF anayejua atusaidie ni kwa nini TRA wanafanya hivyo? Kwa mtindo huu watu wengi wameshindwa kutoa magari yao bandarini kwa sababu wanapokuwa wanaagiza wanajua gari alijazidi miaka kumi lakini TRA ikifika tu miaka kumi, wako na wewe.
Nafikiri hii itakusaidia kuamau ni gari la mwaka gani unapashwa kununua.