Elections 2010 In the last 24hrs: A critical moment for the vital changes--Yes We Can..Yes We Can...

Elections 2010 In the last 24hrs: A critical moment for the vital changes--Yes We Can..Yes We Can...

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Ndugu

Ndiyo sasa tuko kwenye masaa 24 ya mwisho kabla ya kuhitimisha kazi yetu ya kuleta mabadiliko makubwa katika nchi yetu na kuifuta CCM katika historia ya Tanzania. Unaweza kuwa shujaa wa mabadiliko haya...hebu ingia ngomani ucheze.

1. Hakikisha kuwa unatuma sms zisizopungua 100 kuanzia sasa, kuwaeleza watu wako wa karibu na wengine kuwa tunaitwa kutengeneza historia mpya ya nchi yetu kwa kumchagua Dr Slaa na wabunge wa upinzani. Wapigania uhuru wa miaka ya 1960 waliweza. Na sisi pia tunaweza...Yes we can...yes we can..and you can be part of this wonderful moment.
2. Tuma emails zaidi ya 200 kwa watu wote unaowafahamu kwamba muda umeisha, na sasa ni wakati wa kutoa hukumu. Hii ni hukumu ya kihistoria. Kama ilivyokuwa 1961 kwenye historia ya Tanzania, ndivyo itakavyokuwa 2010. Vizazi vyote vijavyo vitaikumbuka na kuienzi tarehe 31/10/2010
3. Msalimie jirani yako (walau nyumba 10) hata kama hujawahi kuongea naye kwa zaidi ya miaka 5 iliyopita. Mfikishie ujumbe huu wa matumaini.
4. Hakikisha unawahi kwenye kituo cha kupiga kura na hamasisha wale ambao una wasi wasi kuwa bado hawajajua nguvu ya kura yao.

Hapa chini kuna baadhi ya SMS unazoweza kutumia.

Hatima ya maisha yako, watoto na hata wajukuu wako iko mikononi mwako na kura yako ndiyo mwamuzi. Mchangue Dr Slaa kwa hatima ya maisha yako na vizazi vyako. Tuma ujumbe huu kwa watu wasiopungua 10

Pia mwingine huu hapa,

Wakinge uwapendao na ccm, vunja ukimya zungumza na CHADEMA,kuokoa Taifa lako linaloangamia kwa ufisadi, badili mfumo na kura yako mpe Dr. Slaa awe rais wako. Usipige kura kwa mazoea...... Tuma kwa watu wasiopungua 10.

Naomba wengine wenye draft sms wanitumie niziweke hapa kurahisisha kazi kwa baadhi ya watu ambao wangependa kuwatumia washikaji zao.


Mungu awabariki sana
Mungu Ibariki Tanzania...Tanzania bila CCM, Tanzania bila Ufisadi...Tanzania bila JK ....inawezekana. Katoe hukumu yako kesho 31/10/2010

Rt Maj Gen. DC(1947)
 
Yes we can! yuko matatizoni kule USA. Siasa za majukwaani na vitendo ni vitu tofauti.
 
Yes we can! yuko matatizoni kule USA. Siasa za majukwaani na vitendo ni vitu tofauti.

Wewe usianze kutuchafulia hali ya hewa. Kama huwezi kuwa sehemu ya mabadiliko una hiari ya kuhamasisha upande wako huo wa mafisadi. Usituwekee usiku hapa. Sorry...
 
mkuu TITLE ya thread havutii watu kuja kuchungulia,

mimi nimetuma watu 20 ambao kura zao bado hazijapata wa kumpa
 
mkuu TITLE ya thread havutii watu kuja kuchungulia,

mimi nimetuma watu 20 ambao kura zao bado hazijapata wa kumpa

Ahsante mkuu.
Ungeshauri title iweje? Hebu pendekeza ili nijaribu kuibadilisha.
 
Back
Top Bottom