Ina maanisha nini pale unampo miss ex wako

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kuna nyakati huenda ukajikuta una mkumbuka au kummiss sana ex wako ambaye alikuwa mtu wako sana na mshirika wako mkubwa


Kitendo cha kummiss inaashiria kwamba upo katika process za kupona na kusonga mbele,kwa maana inaonyesha umekubaliana na ukweli kwamba mapenzi yenu yameisha na inafaa kusonga mbele na kuanza upya.

Hii haimaanishi kwamba utake kurudiana nae na kutaka kuonana nae haraka iwezekanavyo laa,ila ni sehemu ya mchakato wa kupona

Hapa kwanza ni kukubali kwamba uhusiano mliokuwa umeisha ,na kitendo cha kukubali hilo ni moja ya njia kubwa za kupona na kusonga mbele

Lakini vile vile kitendo cha kummiss ex wako ni side effects ambayo ilishajihifadhi katika subconscious mind yako yaan ile sehemu ya ndani ya ubongo ambayo inahifadhi kumbukumbu za kudumu,kwahiyo ni jambo la kawaida tu kwahiyo baada ya mda litafutika na kusonga mbele

Kikubwa ni wakati sasa wa kutafuta furah a yako mpya,ni wakati wa kuona thamani wewe mwenyewe,maana wakati mwengine tunaona thamani yetu pale tunapokuwa na wenza wetu,lakini jua yaliyo pita yamepita,tambua thamani toka ndani yako na baada ya mda utakuwa sawa tu

Hizo hisia za kummiss ex wako zikikujia wala usipaniki na kutaka kumkimbilia na wala usitake kurudiana nae ila kumbuka upo katikati ya kupona na kusonga mbele,be strong haya nayo yatapita

Ni hayo tu!
 
Utofauti upo hapo kwenye kummiss,, binafsi maex zangu huwa nawamiss kwa sababu wengi walikuwa ni wanawake machachari panapo 6*6 nikilinganisha na huyu niliye naye 😎🀝🏽
Yeah ni kweli,kadri jinsi uhusiano wenu ulivyokuwa mzuri na amazing bilashaka hisia za kummiss zitakuwa strong sana,lkn haijalishi uhusiano wenu ulikuwa mtamu kiasi gani,just let go
 
Dah ila wanangu Maisha haya nyie acheni tu. Mara ya mwisho tulipishana na shem wenu miezi 2 iliopita. Tukiwa kirumba akakataa kunipa sukari. Basi tukaachana kihivyo jioni akatembea zake. Toka kipindi hicho hali ni mbaya. Hakuna text, call Wala Nini. Nahisi tumenuniana but niwaambie Nini wanangu... Nimemmis sana shem wenu. Sijui nifanaje.
NB. Sitaki ushauri wa mi kumtext ama kumcall. Bora nijinyonge tu
 
Chonde chondeee
Hala hala dear Exiiiii
Eeee dia exiii
Pole sana mkuu tafuta mwingine namba E tena EJ au EG
 
Kapata mwingine si unajua raha za penzi jipya mkuu ngoja wazoeane anaweza rudi japo sio lazima iwe hivyo.
Dah mkuu basi tu. Kuna muda unajiforce kujifunza kuachana na unaowApenda na ni ngumu kwelikweli but hamna namna. Lazima nikubaliane na jambo hili but nilijiapiza sitatext Wala call Karne Kwa Karne.
Liwalo na liwe.
Nb. Mkuu unaonekana ni popo mwenzangu
 
Hakuna siku mbaya kama siku unayompoteza yeyote umpendae lakini hakuna namna maisha lazima yaendelee.

Soon natoweka mkuu upopo nmeuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…