Kwa vile shirika la ATC ni shirika la umma, mhimili wake mkuu ni serikali.Kwa mujibu wa TCCAA sababu kubwa iliyopelekea kusitishiwa Leseni ni deni la bil.6 inalodaiwa na wadeni wake.
Naomba kuuliza kwa mnaofahamu , hivi ATCL iliwalipa kwanza wadeni wake ndo ikaruhusiwa kuanza safari? Au kinachosikika kwa baadhi ya watu kwamba serikali imeanzisha mmiliki tofauti wa ndege mpya na kujifanya kukodisha kwa ATCL?
Kama shirika la serikali nalo linadaiwa tena zaidi ya hao Fastjet, je, ikisemwa sababu halisi siyo deni bali kubinya wapinzani wa ATCL ibaki peke yake sokoni?
Sent using Jamii Forums mobile app
Fastjet atalipiwa na nani?Kwa vile shirika la ATC ni shirika la umma, mhimili wake mkuu ni serikali.
Shirika hilo lilikuwa na madeni mengi kupita IATA clearance house kiasi cha kufanya code yake isitishwe. Hili ndilo lililofanya shirika hilo kutofanya safari zake kimataifa. Serikali imelipa madeni hayo na hivi sasa ATC iko kwenye mchakato wa mwisho kuweza kurudishiwa hiyo code ili iweze kufanya kazi zake kimataifa.
Wadaiwa ni Fastjet PLC na hii Fastjet ya mheshimiwa inawajibika kuhakikisha hilo deni linalipwa unless kama wanataka kuanzisha airline nyingine mpya ambayo nayo kazi yake siyo ndogo.Fastjet atalipiwa na nani?