Inachukua mawe tripu ngapi kujenga msingi wa vyumba viwili, master bedroom moja, sitting room, kitchen, store na public toilet?

kimara Kimara

Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
80
Reaction score
173
Habari za muda Huu wapendwa,
1000563256.jpg
Kwa wale wazoefu wa ujenzi naomba kujua inaweza kugharimu mawe tripu ngapi kumaliza ujenzi wa Msingi wa Vyumba viwili, master bedroom moja, Sitting Room, dining, jiko na stoo.

Naomba kujuza kwa yoyote mwenye uzoefu maana nilita fundi akanipigia hesabu na kuniambia itagarimu tripu 16 ?

Naomba kujuzwa maana ndio mara yangu ya kwanza kujenga.
 
Habari za muda Huu wapendwa,
Kwa wale wazoefu wa ujenzi naomba kujua inaweza kugharimu mawe tripu ngapi kumaliza ujenzi wa Msingi wa Vyumba viwili, master bedroom moja, Sitting Room, dining, jiko na stoo.

Naomba kujuza kwa yoyote mwenye uzoefu maana nilita fundi akanipigia hesabu na kuniambia itagarimu tripu 16 ? Naomba kujuzwa maana ndio mara yangu ya kwanza kujenga.
Trip 10 mkuu.

Lakini hayo mawe yana changamoto ya ku shake na kusababisha mipasuko.

Ujenzi wa kisasa ni tofari block latio kali za kulaza(kwenye msingi).

Wengine hata kwenye flaw hawagusi mawe, ni kifusi, mchanga na wananalizia kwa zege la kokoto.

Mawe yamekuwa ghali sana bila sababu, nadhani kwa ajili ya soko la ujenzi wa miundo mbinu ya kiserikali.
Chunguza hata majengo ya kiserikali, huwa hawaanzi kujenga msingi kwa mawe.
 
Asante sana, Kwahy ni vyema ujenge msingi wa matofali ? Na je msingi wa mawe, na msingi wa tofali upi ni imara ?
 
Msingi wa matofari ni imara sana, yanalazwa kwa kozi zote za msingi.

Angalia majengo ya Serikali tena yanajengea na wahandisi, hawatumii mawe, wanatumia tofari tu.

Ukiona jiwe kwenye msingi ni kwa ajili ya sakafu.

Ila zingatia, wakati wa kuandaa matofari ya msingi, weka ratio kali, mfano tofari 25-30 kwa mfuko inafaa.

Baada ya msingi ndiyo unaendelea na ratio ya 40 kwa mfuko.
 
Back
Top Bottom