Inadaiwa kuwa TP Mazembe imesitisha nia ya kutaka kumsajili Ibrahim Ajibu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zinameeleza kuwa TP Mazembe wamesitisha nia yao baada ya kushindwa kufikia makubaliano binafsi na mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake na Yanga unatarajiwa kumalizika Juni 30, mwaka huu.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa TP Mazembe wamekumbana na ugumu huo baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba Ajibu alishaingia makubaliano ya awali na Simba, hivyo kama vigogo hao wa Congo watamhitaji wanatakiwa wafanye kwanza mazungumzo na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Mazembe walikuwa tayari kumsajili Ajibu kama mchezaji huru baada ya kuwa na uhakika kuwa Yanga bado hawajamsajili, ila haya yaliyokuwa chini ya pazia, yamewafanya wabadilishe uamuzi wao," kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, bado amekataa kusema lolote kuhusiana na usajili wa Ajibu na kiungo wa Gor Mahia Mkenya Francis Kahata ambaye tayari ameshawaaga wachezaji wenzake wa kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu Kenya.

"Kahata yeye amemaliza mkataba wake na Gor Mahia ndio maana ameamua kuwaaga wachezaji wenzake, kuhusu kutua Simba mimi sijui, nasema subirini kwanza, naona wenzetu (Yanga) wameanza moto na usajili, " alisema Magori.

Msimu uliopita, Simba ilifanikiwa kumsajili Meddie Kagere kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Gor Mahia na mwisho wa msimu aliwaaga wenzake pamoja na viongozi kuwa anarejea kwao Rwanda, lakini siku iliyofuata alitua jijini na kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.
 
Siasa za Simba na Yanga, zinadumaza vipaji. Bora angeenda Mazembe huko huenda angefika Mbali kidogo.
 
Boban
Uncle

Na sasa zamu ya Mzee wa Makorokocho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…