Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Nimefikia eneo hilo na katika stori na wenyeji wanadai tangu nchi ipate uhuru kata hiyo haijapata maji safi na salama jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Kwenye kuzunguka kata hiyo nilifanikiwa kukutana na Wanawake kadhaa wanaopata kadhia ya kukosa maji safi na salama ambapo kwenye kuzungumza nao walidai ya kwamba changamoto ya maji katika kata yao imekuwa kubwa na nilizungumza na wanawake waishio Kijiji cha Imalamihayo ambao walielezea mengi.
Mkazi wa Kijiji cha Imalamihayo, Rehema Simon yeye alisema wanashangazwa na kitendo cha kukosa maji wakati Bomba kubwa linalosambaza maji Tabora likitokea mradi mkubwa wa maji Ziwa Victoria linapita kwenye kiji hicho.
Wanaeleza kuwa barabarani kumekuwa hakuna usalama, mapori ya kutisha lakini kwa kuwa shida yao ni maji wamekuwa wakitembea usiku kufuata maji ili shughuli zingine zifanyike na ndio maisha yao ya kila siku.
Juma Said, mkazi wa Kata ya Uyui anasema Wanawake kwenye kata hiyo wanateseka maana hutembea umbali mrefu zaidi.
Anasema “Kata yetu hii kabila kubwa hapa ni Wasukuma na Kimila Wasukuma huacha shughuli zote kwa Wanawake, sasa apike, afue, alime n.k kiukweli Wanawake wanateseka na kukosekana kwa maji kwenye eneo hili.
“Mbaya zaidi ni kwamba Wanawake wanatumia muda mrefu kufuata maji, hivyo iko haja kwa Serikali kufuatilia na kutusaidia maji kwenye eneo letu hili.”
Watoto nao huathirika na ukosefu wa maji safi na salama.
Kuna wakati Wanawake wanalazimika kuwachukua Watoto wakachote maji, hatua hiyo imekuwa ikiwafanya wengi wao kuchelewa kufika shule na wakati mwingine wanakosa masomo kutokana na kuamka kwenda kuchota maji, wakirejea nyumbani wanajikuta wamechelewa, hivyo kuamua kutokwenda shule.
Wanafanya hivyo kwa kuwa wakichelewa wanaweza kukumbana na adhabu mbalimbali kutoka kwa waalimu wao.
MAMLAKA ZINASEMAJE?
Uchunguzi ambao niliufanya nilibaini ya kwamba Kijiji cha Imalamihayo kina vitongoji 20 ambavyo vinatakiwa kupata maji lakini kati ya vijiji hivyo ni viwili tu ambavyo vimejengwa magati kwa ajili ya kusambazia maji lakini hayajafika, hivyo Wananchi hawawezi kupata maji.
Hata hivyo, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Tabora imeshafuatwa na wawakilishi wa vijiji hivyo mara kadhaa lakini kumekuwa hakuna ushirikiano wa kueleweka ambao angalau ungeweza kutoa mwangaza ni jinsi gai wananchi hao wangeweza kupata maji safi na salama kutokana na bomba kubwa la maji kutoka ziwa Victoria kupita kwenye kata yao huku wakiwa hawanufaiki na maji hayo.
Anachosema Diwani
Diwani wa Kata ya Uyui, Julius Nyanda anasema amejaribu kuzifikisha kwenye vikao vya Halmashauri bila majibu mahususi kutolewa jambo ambalo limewafanya wananchi hao kuendelea kuteseka kwa kukosa maji safi na salama.
Anaeleza kuwa hali hiyo inawafanya watumie maji ya visima ambayo wakati mwingine sio salama kwa kuwa yanakuwa hayajapimwa na wataalamu kuyathibitisha kama yanaweza kutumika na binadamu.
Maji yasiyo salama huweza kusababisa magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine ya tumbo, Serikali ichukue hatua dhidi ya Wananchi hawa.
Pia soma: √ - Tabora: Kata ya Imalamihayo - Uyui maji yapo, bado gati moja katika kitongoji, kazi itakamilika Januari