Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Hii ni kashifa na aibu isiyovumilika yaani Taifa kubwa km TZ tunapeleka wanamichezo 9 kwenye mashindano ya All African Games wakati Kenya wanapeleka 200? Yani mpaka Burundi wanaokatana mapanga kila siku kweli wametuzidi? Waziri wa michezo hv ndani ya baraza la mawaziri huwa anawasilisha hoja gan km haya hayaoni? Na bado anajiita Waziri wa michezo? Sijui anasimamia michezo ipi. Kunatetesi kuwa hata hawa wanamichezo 9 walienda kwa kuungaunga bila bajeti ya kueleweka. Waliishi kwa kukomaa na kwa kujiongeza kiana wao wenyewe. Sawa serikali ina mambo lakini michezo ni jambo la msingi hasa ukiwa na jicho kubwa la kuangalia faida yake kwa ujumla kwa nchi. Kwanza kuitangaza nchi na kuvutia utalii. Kwa mataifa yanayojielewa huwekeza pesa za kutosha katika michezo kwani wanafahamu nguvu yake. Tunalia sn kuzidiwa na Kenya kwenye utalii lakn ukweli ni kwamba wametumia sn riadha,Rugbi,Soka na michezo mingine kujitangaza. Sisi tumekimbilia kuandika slogani za ajabu ajabu kwenye ndege zetu szani km inamantiki yoyote kututangaza nje wakati hata maneno yenyewe hawayaelewi. Michezo huleta ajira. Hebu angalia sekta ya michezo hasa riadha ilivyotengeneza matajiri wakubwa kenya. Tz kwa sasa tunavijana wengi wamesoma lakn hawana ajira. Wakuu wa mikoa na Wilaya wamebaki kutafta kiki kwa kuwakusanya vijana huyu aanzishe mara Intership,mwingine mara semina ya familia nk. Sijui ni nani katuroga. Mpira wa miguu wenyewe ambako kuna afazari ni siasa tupu,Bora hata ndondi wametelekezwa lakn kuna vitu vinaonekana. Serikali hebu oneni wivu,oneni aibu sifa ya nchi na maendeleo hailetwi na madaraja na mabarabara tu. Tunahitaji uwekezaji katika michezo mingine tofauti na Soka. Tutatia aibu aibu kubwa yani kweli kabsa Burundi wanatuzidi????? Naandika huku nateseka sn moyoni. Mafanikio ya michezo yetu imebakia toka enzi za Mwalimu. Tatzo siku hz tumezidisha sn siasa,jambo lolote ambalo kisiasa halina mvuto hata km linafaida kiasi gani ni ngumu kulitekeleza. Elimu bila michezo na uendelezaji vipaji ni sawa na bureee vijana watasoma,na kuishia kurundikana mtaani