Inagharimu sh. Ngapi kutibiwa mataizo ya ugwe mgongo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wanajamvi! Kuna tatizo naomba mnisaidie.
Kuna tatizo lilianza tangu mwaka 2010, miguu ilikuwa inasumbua. Kwenda Hospitali ya Peramiho wakasema Muhimbili ndo wakafanye utafiti zaidi. Nilipuuza kwa sababu uwezo wa kutembea still nlikuwa nao.
Mwaka 2013, miguu ikawa imelemaa...till now kutembea ni issue! Hata usiku kujua mguu uko wapi ni tabu labda mawasiliano hayapo vizuri. Hospitali ya mkoa Morogoro wametoa barua ili niweze kwenda Muhimbili ila kwa sababu mfuko hauko vizuri nimeshindwa kuja. Japo hapa Moro hawajaona tatizo lolote ila wanaamini tatizo lipo kwenye uti wa mgongo.
Kwa sasa nazidi kupoteza mawasiliano.
Mf. hadi mtu anisugue kwa nguvu miguuni ndo naweza kuhisi
Uwezo wa kusikia unazidi kupungua.
Pia uti wa mgongo umeanza kuuma siwezi kukaa nikanyooka
OMBI LANGU KWENU. Kama kuna mwenye kujua tatizo zima la uti wa mgongo linaweza gharimu TSH ngapi? aniambie ili nijipange niweze kufika Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Natanguliza shukrani. AMANI ITAWALE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…