Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Wewe umenunua Passo kuu kuu unakuja kulia lia huku... Tangu lini gari imetembea kilometer kama laki mbili ivi ikawa nzima. Nunua angalau ka Passo kametembea KM elfu sabini angalau na wewe uongeze nyingine hamsini hapo kabla hakajaenda kaburini kuchinjwa skreppa...
 
Kati ya Suzuki Swift, Toyota Passo, Toyota Vitz/Yaris, Honda Fit na Toyota Starlet. Ni baby walker gani ipo imara zaidi, inaweza kwenda masafa zaidi (considering kuwa hizi zote ni town cars). Sijaweka Toyota IST coz nahisi ipo juu ya hizi zote.
 
Umebambikwa kaka,passo zipo za cc 990 na 1290 yakwako sijui ni IPI kati ya hizo.Mbona nilienda na Suzuki KEI cc 660 Arusha zaidi ya km 600 na kurudi haikuchemsha??? Hiyo yako ni mbovu usizichafue Passo,
 
Hivi passo za zambia, congo, rwanda zile IT zinazoshukia bandarini dar huwa zinapelekwaje nchi zao?? huwa zinabebwa na malori au zinaendeshwa??? na je dar lubumbashi au kigali au lusaka ni chini ya km 200???

isijekuwa mtu kauziwa mkweche anatudanganya hapa
 
Zinabebwa kwenye malori ya kubebea magari.
 

Naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…