Inahitaji ujasiri kumiliki PASSO

Kapimwe akili wewe... acha dhalau
Huyu jamaa kama ni dharau hizi za kiwango cha lami
 
Hapa ndo mnapopigwa,mnaamini gari yenye km ndogo ndo nzma,watu wanazirudisha nyuma hizo!Kalaga baho!!
 
Kuchemsha kwa gari ni tatizo linaloweza kutokea kwa gari yoyote ile.
Mara nyingi imettokea hizi gari zinazotumika kwa safari fupi ukibhokoza safari ndefu usipokuwa makini lazima ichemshe.
Muhimu ni kujua gari yako ikoje na hata ikitokea unasafiri safari ndefu lazima uwe na tahadhari.
 
Mpaka kufikia hatua ya kumiliki gari aina ya PASSO inapaswa ujitoe ufahamu mbele ya kadamnasi. Gari gani isiyoweza kutembea 200 kms bila kuchemsha?

Nasubiria tamko/katazo la hizi gari toka ngazi za juu.
Co kwel kk
 
Duuuuuhhh
 
Hizi ni shombo za level yab masters
 
Mpaka kufikia hatua ya kumiliki gari aina ya PASSO inapaswa ujitoe ufahamu mbele ya kadamnasi. Gari gani isiyoweza kutembea 200 kms bila kuchemsha?

Nasubiria tamko/katazo la hizi gari toka ngazi za juu.
Hiyo ina shida
 
Huu ni mtazamo mkuu! na inawezekana ulipata gari ikiwa tayali inamatatizo. Mimi nina Passo kwasasa mbali na nyingine ninazotumia, na nimekuwa nikienda karibu mara mbili kila mwezi Mwanza - Dodoma bila kuhisi hiyo shida ya kuchemsha.

Unaweza kuangalia yafuatayo:
1. Hakikisha rejeta yako imefanyiwa ukaguzi/kusafishwa na mtu ambaye ni mtaalam.
2. Jaribu kuachana na kuweka maji ya Duwasa/Dawasco au kisima kwenye rejeta - jitahidi kutumia coolant. Napendekeza utumie coolant bora sio zile zinazouzwa gerezani. Pata kutoka BP au kampuni nyingine zinazojitambua.

3. Fanya wholesome wngine check - ipimwe system yote. Garage za veta au kwengineko wanaweza kupima gari gako na kukushauri vipuri ambavyo tayali vimechakaa na unahitaji kubadilisha.

Naamini ukifanya haya mkuu wangu, tatizo linaweza kupungua.

TATIZO LA PASSO:
Gari nyingi aina ya Passo zona shida ya usukani kuwa mgumu - kuna indicator moja inajitokeza unapowasha gari "EPS" - ikitokea hiyo unaweza kushawishika kutupa gari kwani hata baadhi ya mafindi wa toyota hasa mikoani hawajui namna ya kurekebisha.

Zaidi ya shida hii sijaona. Kinachonifurahisha zaidi ni kuwa natumia 120,000/- mwezi mzima tofauti na gari zangu nyingine nilipokuwa natumia zaidi ya 250,000/- kwa mwezi (hii nazungumzia Mwanza).

Jitahidi matunzo kwa gari yoyote - utaipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…