Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Historia ya uchumi wetu ni ndefu na isiyo na muendelezo mahususi.Tulitoka uchumi wa soko huria wakati wa uhuru tukaingia ujamaa mwaka 1967, tukarudi kwenye soko huria mwaka 1986 serikali ikiwa bado inashiriki kwa sehemu kubwa kufanya biashara na kushindana na sekta binafsi, mwishowe tukaja kwenye ubinafsishaji mwaka 1994.
Miaka ya 2015- 2021 Tumeshuhudia serikali au taasisi zake zikishirikia pakubwa katika mambo ambayo yalizoeleka kufanywa na sekta binafsi. Hayo ni pamoja na ujenzi wa miondombinu, biashara ya usafiri wa anga, tiketi za Mwendokasi, korosho n.k
Bila kuwa na sera mahususi kuhusu mueleko wa uchumi wetu itakuwa vigumu sana kusonga mbele kwa muendelezo na kasi ya kuwanufaisha wengi.Lazima tuamue uchumi wetu uwe wa muelekeo gani na muelekeo sahihi ni soko huria linaloongozwa na nguvu ya sekta binafsi zaidi.
Mchango na mipango ya serikali katika kujenga viwanda, kumiliki hisa, kuendesha biashara n.k haiwezi kubadilisha uchumi wa nchi kwa kasi na muelekeo sahihi katika kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kuinua vipato, kuongeza ajira na mapato.
Mambo matatu makubwa ya kufanya;
1. Serikali ibinafsishe mashirika na kampuni zote za umma zinazofanya kazi za kibiashara , Hizo ni pamoja na NHC, ATCL, Ranchi za serikali, TANESCO, TBC, BRT, TASAC, Treni n.k Haya mashirika yangweza kuongozwa kwa ufanisi mkubwa zaidi chini ya sekta binafsi kuliko ilivyo sasa.
2. Serikali iondoe vizingiti na "regulations" chungu nzima katika kufanya biashara kupitia sheria, sera, matamko na miongozo yake. Hakuna sababu za kiuchumi za kueleweka kwa nini kuna mlolongo mrefu sana wa kupata passport, kupata vibali vya biashara, kupanga bei za bidhaa, kupanga muda kuuza au kutoa huduma fulani, kuzuia watu kuuza baadhi ya bidhaa zao nje ya nchi wakati fulani, mfumo wa ununuzi mafuta kama BPS n.k Hii inaathiri pakubwa biashara.
3. Ardhi iwe mali binafsi ya watu badala ya mali ya serikali. Mtu kufanya uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu anahitaji uhakika wa kuwepo hapo siku zote. Waziri kuwa na mamlaka ya kutengua umiliki wa ardhi ni jambo linaloweka mashaka makubwa kwa wawekezaji wa ardhi.