Inakuaje gari ni mpya ila namba ni ya zamani

Inakuaje gari ni mpya ila namba ni ya zamani

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Wakuu na wataalam hawa haya maswala, inakuaje gari ni mpya toleo la karibuni lakini namba ya usajili unakuta ni ya mwaka 2001 huko. Naombeni mnijuze
IMG_1170.jpeg
 
Ngoja wataalamu waje,mimi dogo wiki iliyopita kanunua bajaji mpya kabisa lakini kasajili namba D
Nilipomuuliza kasema namba D hazivutii wezi kuiba kama namba E
Aisee
 
Wakuu na wataalam hawa haya maswala, inakuaje gari ni mpya toleo la karibuni lakini namba ya usajili unakuta ni ya mwaka 2001 huko. Naombeni mnijuzeView attachment 2986026
Hiyo ni gari ya Serikali.

Hata plate Number yake huwa ina space ya kuchomeka plate namba nyingine, apart from zile official like STK, STM au STN.

So, huwa wanabandika namba zingine kama hiyo kwa sababu za kiusalama tu.
 
Hiyo ni gari ya Serikali.

Hata plate Number yake huwa ina space ya kuchomeka plate namba nyingine, apart from zile official like STK, STM au STN.

So, huwa wanabandika namba zingine kama hiyo kwa sababu za kiusalama tu.
Hata ukiicheki hiyo plate number hapo inaonekana iko temporarily tu siyo permanent.
 
We jamaa unapigaje gari ya watu number hizo huku mwenyewe kashaaga yuko ulaya
 
IMG_1171.jpeg


Angalia mshale hapo. Pleti namba ni ya kuchomeka siyo ya kufunga na bolti. Kwa hiyo muda wowote anachomoa na kuvalisha nyingine.

Hata gari nyingi za mahakama Kuu na Rufaa huwamwekwa dizaini hii. Ikiwa gari imembeba Jaji huwekwa namba ya J, na ikiwa na shughuli za kimahakama huwekwa namba za serikali.

Kwa ujumla hizi ni gari zenye kazi zaidi ya moja.

Mfano, gari ya Waziri huwekwa namba za Waziri iwapo anafanya kazi za wizara, ila akiwa anafanya kazi za kibunge haswa jimboni huweka namba za private.
 
Kwasababu registration number haimaanishi upya wa gari wala uchakavu wa gari, unaweza kukutana na gari ya zamani na inasoma EAA
 
Back
Top Bottom