Inakuaje idadi ya units za umeme inatofautiana ikiwa gharama ni sawa?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Kwanini gharama za ununuaji wa umeme zinatofautiana kati ya mtumiaji mmoja na mwingine ikiwa wote wana hadhi sawa?

Mfano, mimi nikinunua umeme wa sh.5000 napata Unit 14 lakini jirani yangu akinunua umeme wa kiasi hicho hicho cha fedha anapata zaidi ya Unit 40.

Kwanini TANESCO mmeamua kutoa huduma kwa upendeleo?
 
Mkuu acha na roho ya wivu, kwahiyo unataka hata jirani yako apate unit 14 ili ufurahie. Tambua matumizi yako ni makubwa kwa mwezi ndo maana unapata unit kiasi hicho.
 
Kwa nini gharama za ununuaji wa umeme zinatofautiana kati ya mtumiaji mmoja na mwingine ikiwa wote wana hadhi sawa?

Mfano, mimi nikinunua umeme wa sh.5000 napata Unit 14 lakini jirani yangu akinunua umeme wa kiasi hicho hicho cha fedha anapata zaidi ya Unit 40.

Kwanini TANESCO mmeamua kutoa huduma kwa upendeleo?
Hiyo n i michongo tu, nchi hii hakuna linaloshindikana

kuna kamchongo kwa kuwekwa kwenye category kulingana na idadi ya unit unazotumia kwa mwezi, check na tanesco ofisi iliyo karibu
 
Kwanini gharama za ununuaji wa umeme zinatofautiana kati ya mtumiaji mmoja na mwingine ikiwa wote wana hadhi sawa?

Mfano, mimi nikinunua umeme wa sh.5000 napata Unit 14 lakini jirani yangu akinunua umeme wa kiasi hicho hicho cha fedha anapata zaidi ya Unit 40.

Kwanini TANESCO mmeamua kutoa huduma kwa upendeleo?
Hii inategemea na kundi la matumizi alilopo mteja pamoja na makato yaliyopo kwenye mita husika
 
Hii kitu inanishangaza Kuna rafiki yangu akinunua uneme wa elfu kumi anapata zaid ya unit 60 alafu mimi napata unit 28 aisee sielew
 
Ila hakuna kitu inaumiza Kama kununua luku ya 10000 upate unit 28 wakati wengine umeme wa 10000 unit bwerereee
 
Back
Top Bottom