Inakuaje uchumi wa nchi unakuwa hafu wananchi hawafaidiki

lyaruu01

Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
5
Reaction score
1
Jamani naomba tusaidiane hili, inakuaje uchumi wa nchi unaongezeka lakini wananchi hawafaidiki na kuongezeka huko?
 
lyaruu01,hapa ni Chit-Chat,hii mada yako ungei post Habari na hoja mchanganyiko.
Karibu Jf.
 
Last edited by a moderator:
Jibu rahisi ni kwamba wapo wachache wanaofaidika...
 
Du! Hapa ci mahara pake! Peleka jukwaa la mastress&hasira!
 
Jamani naomba tusaidiane hili, inakuaje uchumi wa nchi unaongezeka lakini wananchi hawafaidiki na kuongezeka huko?

kuna mambo mawili muhimu katika uchumi. Moja ni kukua kwa uchumi na mbili ni maendeleo ya huo uchumi. Hivyo usishangae kuskia ama kuona uchumi wa nchi unakua lakini wananchi hawafaidiki, ni kwasababu hakuna maendeleo ya uchumi licha ya ukuaji wa huo uchumi. Maendeleo ya uchumi ni kama utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi ama jamii, mfano kujenga mashule, kulipa mishahara mizuri watumishi wa umma, kujenga hospitali na vituo vya afya, kujenga barabara na mengine kama hayo. Ni kama wewe uongezwe mshahara alafu badala ya kutumia vizuri nyongeza hiyo ya mshahara katika mambo ya maendeleo ukawa unalewea baa na kuhonga, hivyo mtu mwingine anaweza kushangaa kuona una mshahara mzuri ila huna maendeleo.
 
Kuna utofauti kati ya "economic growth" and "economic development. Sekta zilizokuwa ni utali, miundombinu na kuongezeka kwa wawekezaji kwenye nishati. Sekta zinazogusa watu kama kilimo, Afya na Elimu zinazidi kuporomoka na kwa jinsi hiyo watu tunazidi kuwa masikini.
 
Kukua kwa uchumi (kama kunavyoshabikiwa na wachumi wa economic development kama world bank na IMF) kunapimwa na GDP, ongezeko la pato la taifa linaloakisi uzalishaji. Sasa kukua kwa uzalishaji hakuna uwiano wa moja kwa moja na mgawanyo sawa wa kilichozalishwa na wala hakuna uwiano wa moja kwa moja wa jinsi uzalishaji ulivyotokea katika population husika.

Kwa maana hiyo basi, GDP ikiongezeka aina maana kwamba moja kwa moja mwananchi amenufaika. Kadhalika upo uwezekano kwamba ni sekta chache tu ndio zimesababisha ongezeko hilo.

Wana uchumi wa development economics wao kwa kuondoa mkanganyiko huu wa kukua kwa GDP bila maendeleo ya watu, wakaja na vipimo tofauti vya maendeleo kama vile human development index, social index, human needs index, etc). Udhaifu wa vipimo hivi vya maendeleo ni kwamba vinapima matokeo tu ya zao la shughuli za uchumi bila kueleza jinsi ya kufikia au kupata zao hilo.

Mwisho wa siku, GDP ingawa haionyeshi uwiano wa moja kwa moja wa maendeleo ya watu ni kipimo pekee kinachoonyesha kukua kwa shughuli za kiuchumi katika nchi. Vipimo vingine vinapima matokeo tu ya kukua kwa GDP.

So kwanini kukua kwa uchumi kupitia GDP akuwiani na maendeleo ya watu? Jibu lake ni kwamba GDP inapima kukua kwa uchumi tu na sio maendeleo ya watu. Assumption isiyopingika ni kwamba GDP lazima ikuwe ndipo watu waendelee, lakini sio kila GDP inapokuwa basi watu wanaendelea; kwasababu GDP haina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya watu.
 

Nafurahi umeleta picha nzuri yakueleweka na nimekusoma ingawa sio mleta mada.. Akhsante sana.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…