Inakuaje Wasanii wa Bongo wapewe hela na mashabiki wakati wasanii wa mbele ndo wanarusha hela kwa mashabiki?

Inakuaje Wasanii wa Bongo wapewe hela na mashabiki wakati wasanii wa mbele ndo wanarusha hela kwa mashabiki?

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,863
Ukiangalia shoo za wasaniii wa bongo wakiwa stejini utakuta kuna vijitu vinaenda kuwatuza wasanii kwa kuwapatia hela na msanii utakuta anapokea au anamwagiwa kwa steji yake.

Tofauti naiona kwa wasanii wa mbele utakuta msanii akipanda kwa steji inafikia wakati anatoa bulungutu na kuanza kuwamwagia hela mashabiki. Ni nadra sana kwa mshabiki wa mbele kwenda stejini kumtunza msaniii kama Beyonce, au au Quavo, au Offset, au Kanye, au Jay Z ni kichekesho cha karne, au Nicki Minaji au, Bieber.

Nazani ifike wakati wasanii wa Bongo waache kupokea tunzo toka kwa mashabiki kwani sasahv wanamudu kuwa na ma bodigadi zaidi ya hamsini waanze kuwa wanarusha pesa kuwapatia mashabiki wao ukumbini.
 
Sielewi kwa nini wanagawa pesa wakati wanatoza viingilio ili wapate pesa. Kupokea pesa jukwaani kunaharibu burudani kwa mashabiki lakini.
 
Back
Top Bottom