Inakuwaje CCM waliokuwa hawawataki wapinzani Bungeni, leo hii wawakumbatie Wabunge 19 wa Chadema?

Inakuwaje CCM waliokuwa hawawataki wapinzani Bungeni, leo hii wawakumbatie Wabunge 19 wa Chadema?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Ni dhahiri kutokana na maneno na vitendo vyake, Hayati Magufuli, hakutaka vyama vya upinzani, hususani Chadema, viendelee kuwepo hapa nchini.

Huyo Mwendazake, aliwahi kusikika akitamka hadharani Katika sherehe za kuazimisha, kuzaliwa kwa CCM, huko Singida, akijiapiza kuwa ifikapo 2020, atakuwa ameufuta kabisa mfumo wa vyama vyingi hapa nchini!

Sio yeye tu, bali Karibuni uongozi wote wa juu wa CCM, wamejionyesha kwa matendo yao, kuwa hawaupendi huu mfumo wa vyama vingi, uendelee kuwepo hapa nchini.

Sasa kuhusu hili sakata la wabunge, wanaodaiwa kuwa wa Chadema, huku chama chao cha Chadema, kikiwa kimetangaza rasmi kuwafukuza uanachama wao.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtu yeyote asiye na chama, hataruhusiwa kuwa Mbunge.

Ndipo hapo ninajiuliza, iweje hawahawa CCM, ambao walikuwa wemejiapiza kuwa ifikapo mwaka 2020, watakuwa wameufuta kabisa, mfumo wa vyama vingi na kusalia na mfumo wa chama kimoja cha siasa, ambacho ni chama tawala cha CCM, leo hii wapambane kwa kufa na kupinga, kuwabakiza Hawa wabunge 19, wanaodai kuwa ni wabunge wa Chadema?🥺
 
Back
Top Bottom