Inakuwaje Mwigulu anawadharau na kuwaona Watanzania wajinga? Alituambia tuhamie Burundi sasa hivi anadai tujadili uganga

Siyo anawaona wajinga,ni wajinga kweli.
 
Ni matokeo ya Phd fake za CCM
 
Katika kundi la wajinga ni lazima pawepo na kiongozi wa hilo kundi. Wote ni wajinga ambao wana kiongozi wao. Sasa sijui kama kiongozi amezidisha ujinga ndio maana akawa kiongozi.
 
Rais Samia hataki nidhamu za uoga, waache mawaziri wafanye wanavyotaka hakuna tena kuishi kwa hofu hiyo ndio tafsiri ya uhuru wetu kurudi.
 
Pina anahoja za Kiganga. Amejawa na chuki.
 
Ushamba tu na tabu ya kukulia vijijini huko na kuwa msomi pekee na kila anachofanya anaona yeye tu ndo yuko sahihi kwa kila kitu.
 
Katiba Mpya itapunguza haya majigambo yanayotokana na Pesa walizojichotea kwenye Ofisi za umma.
Dharau Kubwa ni kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata Kutokana na kura za wajinga na wenye mijadala ya Waganga Wa kienyeji.

Dunia nzima watu wanaogombania au kupigania madaraka ni watu Wenye tamaa kubwa ya FEDHA na Mali wakishirikiana na Wasomi.
Kinachowadhibiti ni Uimara Wa Katiba au SHERIA zinazobana na kuhoji Mali za Viongozi.
Bila Katiba mpya Hawa CCM watatupiga,KUTUKANA ,kutudharau,kutukejeli,kutudhalilisha, kutufokea,kutugandamiza kuliko Wakoloni.

Hawa vijanaMakamba ,Mwigilu, Riz one n.k. ni Vijana wanaoshindana ,kujitangaza ,kukusanya Mali na FEDHA Kwa ajili ya uchaguzi 2030.

Nape ni KIJANA asiye na tamaa lakini ana Maneno yasiyofaa kama Mwigulu ndivyo yanayomgharimu.

Ndani ya CCM na SERIKALI yake Kuna Vijana Bora Wenye sifa .Pia ndani ya baraza la mawaziri wapo lakini Kwa Katiba hii ya Kikoloni hawafai kuongoza nchi. NJE ya baraza la mawaziri pia wapo Vijana Bora ZAIDI ila Kwa Katiba hii wataharibu mana wanauwezo Mkubwa Wa kutawala kuliko kuongoza . Mfano Paulo Makonda, RC.Antón Mtaka, RC.Chalamila ,DAS . JOHN Nchimbi wote ni Vijana Wenye uwezo mzuri na Wenye maadili ya Kiafrika lakini Kwa Katiba hili Tulio nayo Hawa Vijana hawataweza kuongoza na kuonyesha uadilifu Wao. Ni Katiba ya Kikoloni inayolinda maslahi ya Wachache walioko kwenye madaraka na waliowahi kukalia madaraka na familia Zao. Kuendelea kuikumbatia Katiba hii ni janga kubwa sana Kwa Ustawi Wa watu mil. 61. Katiba inayolinda maslahi, vyeo na MAISHA Bora Kwa watu wasiozidi Elfu tatu tuu.
Yaaani, Katiba ya kulinda maslahi ya Wabunge, mawaziri na manaibu, wakuu Wa mikoa,maDC, Wakurugenzi, majaji, wakuu Wa vyombo vya Dola, Rais na Makamu wake ,Waziri mkuu, Spika na wakuu Wa Idara na mabalozi, wastaafu Wa chama na SERIKALI na familia Zao basi.Hawa NDIO Wanaoshirikiana na matajiri Wa ndani na NJE kuvuna maliasili za Taifa hili ,Hawa NDIO waliojificha Nyuma ya Kila biashara iwe Haram au halali,(huwezi kuunganisha bomba la mafuta Kwenda Nyumbani Kwako Bila Hawa kushiriki) . WENGINE wote kwenye nchi hii ni waokota makombo na wapiga miayo tu Hata kura za wengine hazihesabiwi. Kura zinazohesabiwa ni za Hawa wasiozidi 1% ya watanzania mil.61.

Ni lazima wananchi waamke Kupinga hili kundi dogo sana la wanyonyaji kupitia madaraka. Hawa wamenyonya mpaka Viinua mgongo vya Walimu, viinua mgongo VYA Mapolisi, Viinua mgongo VYA wanajeshi wore,Viinua mgongo VYA askari Wa Magereza n.k. Ni kundi lenye ulaghai Mkubwa Wa kugandamiza wafanyakazi wote Kwa vitisho VYA kuwafukuza KAZI Huku Wakiwa wanajua kuwa njaa ndiyo Silaha Yao kubwa. Wanaogelea JUU ya FEDHA na utajiri Wa kutisha kupitia ofisi za umma Huku watumishi WENGINE Wa chini Wakiwa na umaskini Wa kutisha.
Hawa asilimia moja NDIO wakishirikiana kutunga Sheria za Plea bargain na kuweka watu wao Wa kuteka watu na kupora FEDHA za wafanyabiashara. Haka kakundi kadogo Leo kanapaka watu mafuta Kwa mgongo Wa chupa Kwa kusema kuwa pawe na Kodi rafiki Huku wakijua wazi kuwa wamewafilisi wafanyabiashara Wa Kweli na Sasa wao NDIO Wenye FEDHA wanaweka wawekezaji Kwa mlango Wa Nyuma na kujipa unafuu Wa Kodi.

Wanapeana madaraka Kwa lengo la kula na kuvimbiwa Huku mishahara ya wafanyakazi Wengine IKIWA Duni . Wakiulizwa wanasema fungu kubwa la Kodi ya wananchi linaishia kwenye Mishahara ya wafanyakazi Bila kusema ni fungu kubwa kiasi Gani linaloishia Kwa watawala na wakuu Wa Idara wasiozidi 5000 kati ya Wafanyakazi ZAIDI ya Milioni moja Wa umma.

Ni Wakati Sasa Wa Wapinzani Wa Kweli kuungana na wale waliopo NDANI ya CCM wanaokerwa na matumizi mabaya ya Mali na utajiri Wa nchi hii kupitia Katiba mpya.
Lakini pia wananchi tuungane Kudai Katiba mpya inayotokana na Maoni ya wananchi. Maono ya watawala ndiyo kama ya Mwigulu. Wananchi wanawakilishwa na wabunge. Sasa wabunge wameambiwa na SERIKALI kuwa uwezo wao ni Wa kujadili mambo ya Waganga Wa Kienyeji basi.

Kuhusu Katiba Mpya ni Bora Mama Dr Samia 2025 apite bila kupingwa lakini atupe Katiba mpya. Taifa litakua limeweka misingi Bora Kwa lila mmoja kulitumikia Taifa lake Kwa uadilifu na Kwa moyo.
Katiba mpya inafaa sana kwa kiongozi mwanye utashi Wa maendeleo lakini pia kusimamia Haki Kwa watu wote. Sifa hii anayo Mama Samia Lakini Kwa Katiba tuliyonayo ni Bora pawe na Rais mwenye hulka ya Kikoloni mana Katiba tuliyo nayo ni katiba ya SERIKALI ya Kikoloni. Ukoloni unaendeshwa Kikoloni na kidhulma dhulma na ukatili na ubabe Kwa KUTUMIA vyombo VYA Dola.
Katiba tuliyo nayo ni muafaka kabisa Kwa watu kama Mwigulu Nchemba.

Tumsaidie mama alete Katiba mpya Ili atimize Azma yake ya kujenga Taifa lenye misingi ya Haki na usawa Kwa wanadamu wote Kwani wote ni waja Wa Mwenyezi Mungu.
 
Mwigulu kamuweka Samia kwenye kiganja chake,ndo maana anajiamini kutukana watanzania kama anavyotaka.
Daah jamaa anatukana aisee hapo anatumia kodi za Wananchi angekua mfanyabiashara harafu kafanikiwa ingekua shida zaidi...
 
Mtoto pendwa aliyeshika kibubu !
 
Kwa sababu wewe na wenzio ni wajinga na mbumbumbu wa Uchumi.
Para SoMo hapa kutoka Kwa Mwigulu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…