Inakuwaje nyama ya baa inakuwaga nzuri zaidi ya nyama ya home, hata ya home ipikwe fresh zaidi?

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,465
Wakuu. Nipo hapa napiga Ile nyama pendwa leo
Sasa najiuliza iweje ya home inaandaliwa kwa usafi na kwa kiwango ila hii ya huku kwenye makuti, kachumbari sijui ilitengenezwa akiwa na makamasi ila ndo tunayoikimbiliagaaaaa!!!!

NB: Hata soda iwe home

Hata bia ikiwa home inakuwa haina utamuuu hii ikoje?
Wakuu hata mechi ya mpira ikiwa home hainogi ng'ooo
 
Mmmmmh wewe ngoja waje wadau
 
Aaa wapi... mindset tuu, sijawahi ona vyakula vibovu kama vya kununua... chakula hujui nyama ni ya kibudu au kiumbe hai?
Hujui ni nyama ya mnyama gani sasa nn hyo? kimekaa siku ngapi? packaging etc
-Hujazungumzia maswala ya usafi na usafi mhudumu mwenyewe.
-Mainzi yanatapakaa... vyombo navyo kila mtu anatia maudenda yake...

Pengine mkuu kwenu hamjui kupika usilinganishe na wengine.
 
Labda mpira nakuunga mkono coz bila washabiki kitu hainogi.
 
SIDHANI MKUU.MI NADHANI YA BAR UNAONA TAMU KWA VILE UNAPENDA ULE PEKE YAKO NA SIO NA FAMILIA
 
Hamna kitu napenda kama beer na nyama za kutayarisha nyumbani..... Sijui wewe nyumbani kwako wanapika vipi..... Ila kwangu wanajua kuanzia michemsho, kuchoma, kukaanga na korokocho nyingine. Yaan nina nimezungukwa na watu wanajua mapishi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…