Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,851
- 9,472
Habari zenu wapenzi wangu wote wa MMU??
Hili jambo nimelifikiria kwa muda mrefu, na kila siku nazidi kulifikiria ila nakosa jibu. Watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano eg wapenzi, inapotokea wamegombana wanatafuta mtu mwingine awasuluhishe na mara nyingi huwa anafanikiwa. Swali ninalojiuliza, inakuwaje mwanamke/mwanamme haupo tayari kumsikiliza mwenzio na kumuelewa ila upo tayari kumsikiliza mtu wa pembeni? Hivi inaleta picha gani baada ya nyie kupatana baada ya kusuluhishwa na ndugu au rafiki?
Binafsi nafikiri kama mpenzi wangu hatonisikiliza mimi, sitokuwa tayari amsikilize mwingine kwa niaba yangu na kama sipo tayari kumsikiliza yeye na kutatua tatizo basi sitoweza kumsikiliza ndugu wala jamaa yake. Wewe je unaonaje?