Inakuwaje ugomvi wenu wa mahusiano utatuliwe na wengine...????

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
23,851
Reaction score
9,472
Habari zenu wapenzi wangu wote wa MMU??
Hili jambo nimelifikiria kwa muda mrefu, na kila siku nazidi kulifikiria ila nakosa jibu. Watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano eg wapenzi, inapotokea wamegombana wanatafuta mtu mwingine awasuluhishe na mara nyingi huwa anafanikiwa. Swali ninalojiuliza, inakuwaje mwanamke/mwanamme haupo tayari kumsikiliza mwenzio na kumuelewa ila upo tayari kumsikiliza mtu wa pembeni? Hivi inaleta picha gani baada ya nyie kupatana baada ya kusuluhishwa na ndugu au rafiki?
Binafsi nafikiri kama mpenzi wangu hatonisikiliza mimi, sitokuwa tayari amsikilize mwingine kwa niaba yangu na kama sipo tayari kumsikiliza yeye na kutatua tatizo basi sitoweza kumsikiliza ndugu wala jamaa yake. Wewe je unaonaje?
 
MMU leo pasua kichwa ngoja nijipange nirudi na mauzoefu
 
Mie naona kama unavyoona.

Halafu hii tabia ya baadhi ya wanaume kusambaza taarifa za ndani ya nyumba zao au mapungufu ya wake zao kwa ndugu zao ndio inayosababisha ndugu waanze kumchukia mkeo, mpenzio.

Ukiingia kwenye mahusiano ikiwamo ndoa, jua fika umekuwa mkumbwa na umeanza familia ambayo ni baba, mama (na watoto kama mtabarikiwa). Aibu yako ni aibu ya familia na aibu ya familia ni yako.
 
naungana na wewe husn! Matatizo ya wapenzi/ mke na mume inabidi wayamalze wenyewe wakishindwa cdhan kuna atakayeweza. Naendelea kutafakari zaidi.
 
Ni kweli siri za ndani inatakiwa zibaki ndani hivyo wanandoa ni vizuri kumaliza tofauti zao wenyewe kwa wenyewe. Lakini kunawakati migogoro inakuwa mikubwa zaidi hivyo huitaji huitajika busara zaidi kutoka nje, lakini ni vizuri mambo yamalizike ndani kwa ndani ikishindikana basi wazee ktk familia wahusishwe.
 
Watu wengi sana wanapenda kutatuliwa matatizo yao badala ya kuyatatua wenyewe!!Binafsi sifagilii...kama uneweza kuyaanzisha uweze pia kuyamaliza!
 
Listen my dear, tatizo ni misunderstanding. Kuna wachache ambao huwa wanaweza kuji-express na kuelewana wenyewe, lakini baadhi ya watu huwa ni wagumu mno kuelewa. Hapo ndipo mtu wa tatu hutafutwa kwa lengo la kuwasikiliza waliogombana na kujaribu kuwaeleza wote wawili jinsi alivyowaelewa. Wakishaelewa wote wawili, huwa ni rahisi kupata suluhisho, iwe kwa wao wenyewe, au kupewa alternative na mtu wa tatu!
 
Mi naunga mkono wachangiaji hapo juu kwamba mkikwaruzana tafuteni suluhu wenyewe haina haja kutoa siri zenu kwa wengine
lazima mmoja ajishushe ili mfikie mwafaka msitumie ubabe hata kama ni mwanaume jishushe au mwanamke ili mfikie suluhu
mkitoa siri zenu nje tayari hapo familia inaingia kwenye matatizo hata hao wazee siku hzi sio wale wa zamani siku hzi unaweza
kumwita mzee ukifiri ana busara kumbe anaenda kuzambaza huko nje deal with the problem on your own...
 
Reactions: BAK
lazima mmoja ajishushe ili mfikie mwafaka msitumie ubabe hata kama ni mwanaume jishushe au mwanamke ili mfikie suluhu
nafikiri hiyo ni namna nzuri ya kufikia muafaka.
 
halafu wewe hiyo miguno,..

Huo mguno ni ishara kuwa the boss matatizo yake anayapeleka kwa majirani zake!

Mi bado siafiki hili swala la kupeleka matatizo nje yenu. Naungana na Lizzy alvyosema kama unajua kuyaanzisha, ujue na kuyamaliza pia...
 
hata mimi ninawashanga watu kama hao, na kweli haifai.., lakini watu wengine huwa wanaona hawajafanya Kosa au wanaona wanaonewa mpaka wasikie from the third party... lakini my motto is......

"Never tell your problems to people.., Many Dont Care.... others are Glad that you have Them, and the rest Have more problems than you.....
 
Reactions: BAK
mimi matatizo yangu namwita lawyer tu lol

hisia zenu zipo njenje hivyo
 
mi pia jaman hii tabia siipend kwel kama uliweza kunitongoza kwa nn tukikosana uniogope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…