Inakuwaje wanajeshi (JWTZ) wanalinda Fiesta?

Inakuwaje wanajeshi (JWTZ) wanalinda Fiesta?

Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Posts
7,988
Reaction score
4,508
Redio Clouds wanatangaza kuwa kwenye show lao Leaders Club linaloendelea saa hizi kuna ulinzi wa uhakika pamoja na polisi wana ulinzi wa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.

Hii imekaaje wanajeshi kulinda onyesho la mziki ina maana polisi hawatoshi au wanajeshi wamependa kuwa pale kwa malipo maalum,
nilikuwa sijui kama mtu yeyote anaweza kukodi wanajeshi (JW) na wakamfayia ulinzi, ila nafikiri ni aibu kwa jeshi letu.
 
Nimesikia clouds wanatangaza Fiesta pale Leaders Club inalindwa na JW kwa nini wanajeshi wetu wanajidhalilisha kiasi hiki tatizo nini au mishahara haitoshi tuelezane.
 
Nafikiri clouds waombe hata na helcopter geshini
 
hivi tatizo liko wapi? ...wanajeshi wafanye kaz gani jamani? waache watulindie dada zetu ,kaka zetu na wadogo zetu.. kwani wanawalinda wakenya au wahindi?
 
Ni ujinga na udhalishaji kwa jeshi kufanya kazi za watu binafsi, cdf atawajibika kwa hilo kama ni kweli?
 
siwaungi hoja clouds fm..kwahiyo wanataka kutuhakikishia kwamba wao wanauwezo wa kulipa kazi jeshi letu,..lol nahodha na mwinyi kazi imewashinda
 
kwa tanzania lolote lawezekana!hukuona masandukuru ya kura kuibwa na jwtz?
 
Yahani watu tunaibiwa huku majumbani hawatulindi ila fiesta ndo bora!
 
hivi tatizo liko wapi? ...wanajeshi wafanye kaz gani jamani? waache watulindie dada zetu ,kaka zetu na wadogo zetu.. kwani wanawalinda wakenya au wahindi?
Tusichukulie kila kitu simple eti walinde dada zetu polisi wafanye kazi gani, kazi ya jeshi JW si kulinda kumbi za starehe ni kulinda mipaka ya nchi labda na kusaidia kwenye majanga litakapoombwa ingawa pia hiyo si kazi yake. Mwanajeshi anatakiwa awe kambini wakati wote hata kama hana kazi kwa sababu wanalipwa hata wasipofanya kazi, kwa nchi zinazofuata utawala wa sheria hii ni kashfa lakini kwetu kinaonekana ni kitu cha kawaida.
 
mimi pia nimesikia hii thru clouds radio.. kama ni kweli, NI FEDHEHA KWA JESHI..nafikiri moja ya kazi za jeshi ni kulinda mipaka ya nchi dhidi ya maadui..hili la kulinda kumbi za starehe hapana...
 
Dah' kweli cluds ni ccm damudamu' ndo maana wanamwandaliaga Amri jeshi mkuu sherehe za Birthday yake,nadhan amewapa bakshishi! SHEREHE ZA CCM KIBONDE NDIYE ANAKUWAGA 'MC'. Hvyo wanapeana 'turff'
 
Ni ujinga na udhalishaji kwa jeshi kufanya kazi za watu binafsi, cdf atawajibika kwa hilo kama ni kweli?
Ni kweli ndugu yangu nimesikia mimi niko nje kikazi nasikiliza clouds online mtangazaji amesema kuna safu 5 za ulinzi kwanza
jeshi la polisi,
Ninja,
Bouncer,
Jeshi la wananchi Tanzania na
askari wenye nguo za kawaida(plain clothes cop)

nimesikitika sana ni aibu na ni kulidhalilisha jeshi letu kuwa ni la njaa, ina maana mimi nikiwa na harusi yangu nikifika bei nawakodi JW.
 
Back
Top Bottom