Inama Diamond kamuimbia Zari!?

Storm shadow

Senior Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
167
Reaction score
132
Habari za muda wakuu,

Katika kusikiliza na kusoma lyrics za ngoma ya Diamond Platinumz Ft Fally Ipupa inaonekena aliamua kufikisha ujumbe kwa mzazi mwenzie huyo.

Tuanze hapa

"Una pesa kama Dangote unaeza penda mtu yeyote" mwana mama Zara amekuwa akitamba katika interview kadhaa kuwa yeye ana pesa ikiwemo ile na Millard Ayo

"Mapenzi sio sumu kasome kwa kitabu" hapa jamaa kaamua kumpa message mzazi mwenzie huyo baada ya kuonyesha kumchukia

"Siku hizi wanangu siwaoni naishia kuwa like insta" hii no baada ya Zari kuzuia jamaa kutopata nafasi ya kuwaona watoto wake

"Anaekupenda pendana nae asokupenda acha nae " baada ya Zari kuonesha kumchukia kupita kiasi ukizingatia jamaa alikiri kuwa mzazi mwenzie huyo alichepuka alipokuwa akihojiwa wasafi FM block 89 na jamaa kuwa na mahusiano na Tanasha
 
Dada yangu baada ya kuparaganyika na aliyekuwa mume wake alikaa na watoto na kufanya kila aliloweza kumzuia baba wa watoto wao asiwaone wala kukutana nao, nilimshauri saana asifanye vile kwakuwa walipata watoto wale kwa pamoja akakataa.


Amehangaika sana kuwakuza kwa taabu mno! Shule kulipia ada ilikuwa patashika nguo kuchanika hadi anatuomba kaka zake tumsaidie.

Watoto wamekua na wao wenyewe kwa utashi wao wakamsumbua sana mama yao baba yuko wapi? Mwishowe wamekutana na baba yao na wanashirikiana nae vizuri tu bila tatizo lolote lile, mama yao akiwalalamikia wanamwambia ni baba yetu kama ugomvi ni wa kwenu nyie sisi hautuhusu


*Do not destroy relationship beyond repair, dunia tunapita
 
ahsante mkuu kwa somo
 
Mkuu mbona domo hajamsamehe baba yake na kumpa bata ndefu kama za anko shamte
 
Ahaaaah hata ujui nyimbo ikoje correction
Mapenzi sio somo kasome kwa kitabu eboooooh nasio sumu eboooooh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…