Inaonekana watu wamekubali tozo za miamala

Inaonekana watu wamekubali tozo za miamala

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Mwezi wa Saba serikali iliweka tozo kwenye miamala ya simu na kukawa na lawama nyingi sana huku wengi wakiamini wananchi wangeacha kutumia huduma hiyo ya kutoa na kupokea fedha.

Hata hivyo kwa kutumia takwimu inaoneshwa wananchi walisusa kidogo halafu hali imerudi kama kawaida watu wameanza kuzoea na wanaendelea na huduma kama kawaida.

1652335872140.png

Takwimu zinaonesha mwezi Juni hadi septembe pesa zinazotumwa na kutolewa kwa njia ya simu ilipungua kwa kiasi kikubwa lakini ilirudi kuwa kawaida kuanzia mwezi Oktoba na imepanda sana Desemba.

1652336015665.png

Hata hivyo bado miamala iko chini ya kiwango kilichozoeleka na hii inaonesha athari kubwa. However, inaonekana wananchi wameanza kukubaliana na hali iliyopo

Data Source: BoT
Graphs katengeneza Mkoba Mfuko
 
Utachagua ugomee tozo ya muamala au tozo za mafuta. Chaguo ni lako
 
Miamala inaweza kuwa mingi lakini amount ikawa ndogo. Yote kwa yote watanzania ni wasahaulifu hivyo wataendelea kutumika.
 
Wazee wakupika data ww hyo graph huwezi kuchora mnaamini huo uongo wakati ukweli unajulikana.
 
Wazee wakupika data ww hyo graph huwezi kuchora mnaamini huo uongo wakati ukweli unajulikana.
Aisee unanifahamu sana. But pia inaonesha ufahamu wako uko limited sana
 
Miamala inaweza kuwa mingi lakini amount ikawa ndogo. Yote kwa yote watanzania ni wasahaulifu hivyo wataendelea kutumika.
Hiyo sio idadi ya miamala bali Volume(Kiasi) ya miamala,
 
Back
Top Bottom