SoC03 Inapotokea njaa nchini sababu

SoC03 Inapotokea njaa nchini sababu

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 24, 2016
Posts
15
Reaction score
10
Draught weather for human photos 2.png


Baada ya kuona ugumu wa maisha nchini, Kama Mtanzania, Mzalendo, nikaamua kuingia mitandaoni kutafuta na kujua sababu yake ni nini? Nilipopitia baadhi ya mitandao ya kitaifa na kimataifa. Nimekuta habari za sababu ya kuwepo kwa njaa katika baadhi ya maeneo nchini.

Sisemi kwasasa kuna njaa na uhaba wa chakula ila kuna ugumu wa maisha katika familia mbali mbali. Ndicho kilichonivuta kufanya uchunguzi kidogo kupitia mitandao mbalimbali na kubainisha walichokiandika kulingana na tafiti na vyanzo vya habari walivyokuwa navyo.

Wao walibainisha kunasababu saba ambao nitakwenda kuzioredhesha ili tuone na kujadili kwa pamoja ndizo zinazoleta njaa na uhaba wa chakula nchini na kufanya maisha kuwa magumu?

Ifahamike kuwa hizi ni sababu za ndani sijazungumzia zile za nje yaani kimataifa. Hivyo msininukuu vibaya na wala sina mlengo wowote ninaosimamia ni mapenzi mema ya nchi.

Na kuona kuwa Watanzania tuna uwezo mkubwa hata kuilisha Afrika nzima bila shida kabisa, ndiyo nikaja na Makala hii.

Tuanze kwa kuona walichosema wao walianza kama hivi: Sababu ya kwanza;


1. Ukosefu wa ajira​



Hapa nikajiuliza sana mbona kila kukicha naona vyombo mbalimbali vinatangaza nafasi za kazi za elimu ya juu na hata za wa elimu ya chini nina maana ya kazi za kutumia nguvu Zaidi siyo ujuzi.



Sasa nikajiuliza kama kazi zinatangazwa kwa wingi hivyo tatizo linaweza likawa wapi? Ndiyo maana ya kuamua kuchukua kalamu na karatasi kuandika Makala hii tuweze kujadili kwa pamoja sababu ya njaa kweli ni kukosa ajira.?



2. Mabadiliko ya hali ya hewa​


Unaposoma vitabu vya kiimani kwa mfano Biblia takatifu naitaja hii kwasababu ndiyo ambayo nimebahatika kuisoma na huwa naisoma mara kwa mara. Yenyewe inaonyesha kwamba Mungu aliumba Dunia na kumkabidhi mwanadamu aitawale.

Sasa hoja yangu hapa kama kitu unakitawa, kama kutakuwa na shida inakuja si ni lazima utakuwa na taarifa yake. Kama utakuwa huna taarifa yake hilo ni tatizo.

Sasa kwanini mabadiliko ya hali ya hewa yatokee na huyo mwanadamu asiwe na taarifa wala suluhisho ambalo amejiandaa nalo baada ya matokeo ya mabadilko hayo.

Nayaleta haya kwenu tujadili inawezekana mimi mawazo yangu yako chini hivyo wengine mnaweza kuinua Zaidi tukapata njia ya kupita katika hili.


3. Mfumuko wa bei​


Hali hii ni sababu ya kuleta njaa nchini katika baadhi ya maeneo? Mimi siyo mtalaamu wa mambo ya uchumi. Nilisoma kidogo katika kozi yangu ya uandishi wa habari za biashara za kiuchunguzi na sikubobea sana.

Naamini mtakaosoma Makala hii wengine ni wabobevu wa masuala ya uchumi hivyo mtachangia hapa kutuambia kama ni moja ya sababu za kuleta njaa nchini.

Na jinsi ya kuweza kuepukana na sababu hiyo isiweze kuumiza wananchi Zaidi katika maeneo yetu yote. Naongelea mijini na vijini wanakoishi Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao.



4. Ukame uliokithiri katika baadhi ya maeneo​


Hapa nilijiuliza tulivyo na ukubwa wa eneo hapa nchini lakini ukubwa uliyopo wa eneo linalofaa kwa kulimwa mazao. Sikuishia hapo nikatazama jinsi tulivyo na uwingi wa mito inayotiririsha maji katika Bahari ya Hindi.

Niakasewaza kwa sauti kusema kwanini hapa ukame utuzidi maarifa?

Nadhani si kweli kwamba ukame unaweza kutuzidi maarifa. Lakini tujiulize ndiyo iwe sababu ya kutukosesha sisi kuweza kuendelea na kilimo cha umwagiliaji? Na kwa bahati nzuri ukame huwa haukumbi Tanzania nzima ni baadhi tu ya maeneo.

Je wakati wa msimu wa mvua hayo maji ya mvua je hatuwezi kuyatunza yakatusaidia wakati wa ukame? Hapo mimi nawaza nategemea wewe nawe utachangia kwa maoni yako, ukame unaweza ukatushinda Watanzania tusiweze kulima kabisa?



5. Magonjwa ya mazao na wadudu waharibifu​


Bado narudi katika uumbaji, Mwanadamu aliweza kupewa uwezo mkubwa sana kuweza kutawala na kuitishaa nchi. Hivyo sidhani kama magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao wanaweza kusimama mbele ya mwanadamu mwenye mamlaka yote.

Nafikiri kuna sehemu tunashindwa kusimama na kuitumia mamlaka tuliyopewa na Mungu. Au wenzangu mnaonaje? Nimesema maoni yanaruhusiwa, mimi nimeanzisha mjadala tu kuangalia na uwezo tulionao Wanadamu kwanini tuendelee kulia njaa au maisha magumu?

Magonjwa ya mazao na wadudu kweli iendelee kuwa chanzo cha Watanzania kupata njaa, mimi nafikiri tunaweza kuwatiisha hawa tena na kuwatokomeza kabisa wasionekane katika mipaka ya nchi yetu.


6. Utumiaji mbovu wa chakula​


Sidhani kama mtu ametaabika kulima na kupata mazao yake vizuri. Labda ni mwenye matatizo ya akili tuu anayeweza akashindwa kutunza vizuri na kukitumia kwa utaratibu. Bahati iliyopo nchi yetu ardhi yake imebarikiwa kwa kuzalisha mazao yote ya biashara na ya chakula.

Na Watanzania tunavyoishi kwa umoja huzuiliwi kwenda kuomba au kukodi ardhi Mkoa wowote ule uweze kulima mazao ya kutosha ya chakula kwa matumizi yote, lakini mazao ya biashara kwa matumizi ya kujipatia kipato.

Sasa utumiaji mbovu unatoka wapi? Au kuna kitu mimi sikijui hebu toa maoni yako hapo chini ili kuboresha hali ya kupambana na hizi sababu za kuleta njaa na ugumu wa maisha hapa nchini. Nafikiri kwa pamoja tunaweza hakuna sababu ambayo itasimama hata kama ni ya nje.



7. Matumizi yasiyofaa ya pembejeo za Kilimo


Bado narudi pale niliposema Mwanadamu alikabidhiwa nchi na Mungu na akapewa mamlaka ya kuitiisha na kuvitawala vyote viijazavyo. Hivyo matumizi yasiyofaa hayawezi kuwepo kwa mtu ambaye anatumia mamlaka vizuri aliyopewa na Mungu.

Lakini amefundishwa na wanadamu wenzake, kwa maana ya watalaamu lakini pia hata yeye amekwenda shule ameondoa ujinga, hivyo hawezi kuwa mzembe wa kiasi hicho.

Sasa hapo matumizi yasiyofaa yanatokea wapi? Labda uniambie hakuna pembejeo za kilimo za kutosha hilo ni jambo lingine. Mimi kinachonishangaza ni kwamba pembejeo unazo halafu wewe unatumia ndivyo sivyo.

Hapa sioni kama hii sababu inaweza ikasimama na kuwa chanzo cha njaa nchini. Isipokuwa nafikiri tumezoea kutafuta sababu za kujitetea pale inapotekea njaa pengine hata kwa uvivu tuu.

Nafikiri twahitaji mabadiliko ya kuangalia suluhu ya jambo Zaidi, kuliko kubakia kuangalia sababu na chanzo chake. Maana haya siyo ndiyo sasa yanatokea hatuyajui, yamekuwa yakitokea tangia misingi ya Dunia hii ilipoumbwa na kupewa Mwanadamu aitawale.

Yamekuwa yakitokea pale Mwanadamu aliposhindwa kusimama katika nafasi yake ipaswavyo.

Mungu akamwita uko wapi? Akasema tuliposikia sauti yako tukajificha! Sababu ya kujificha ameharibu na hataki kutengeneza. Tunazijua sababu zinazotuletea njaa na ugumu wa maisha tujiandae basi na suluhisho, siyo tena kubakia kuangalia sababu kila mwaka.

Au mwenzangu unasemaje? Tukishikana kutafuta suluhu hizo sababu zitasimama? Karibu kwa maoni, mapendekezo, ushauri hata kumkosoa Mwandishi wa Makala hii.
 

Attachments

  • Draught weather for human photos 2.png
    Draught weather for human photos 2.png
    251 KB · Views: 2
Upvote 1
Tubadilike tujifunze iweje Israel ni jangwa ila inalisha waarabu wenzake.
 
Tubadilike tujifunze iweje Israel ni jangwa ila inalisha waarabu wenzake.
Ndiyo maana nimeuleta mjadala hapa. Sina uzoefu na kilimo cha Israeli jangwani, kama unauzoefu japo kwa ufupi tupe hapa. Watu wengi wanataka kujifunza ili tuache tabia ya kutoa sababu na tuone jinsi tulivyo barikiwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom