- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Dakika chache baada ya ndege hiyo kupotea katika rada, hichi ndicho walichoposti jeshi Israel katika ukurasa wao wa X.
- Tunachokijua
- Bashar alikuwa rais wa Syria kuanzia mwaka 2000 mara baada ya kifo cha baba yake aliyehudumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 1971. Uongozi wa Bashar ulishutumiwa kama uongozi wa kiimla nchini Syria ambapo amekuwa akihusianishwa kutokuwa na utofauti na kiongozi aliyepita kabla yake ambaye alikuwa ni baba yake mzazi Hafez al-Assad.
Bashar al-Assad nafasi yake ya kuonekana kuwa mrithi wa baba yake katika uongozi ulionekana mara baada ya kaka yake Basil al-Assad kufariki dunia kwa kile kilichodaiwa ni ajali ya gari iliyotokea januari 21, 1994. Kutokana na kifo cha Basil ilibidi mtoto mkubwa wa pili wa Hafez al-Assad ambaye ndiye Bashar ajiandae kurithi nafasi ya urais wa baba yake, na hivyo Bashar akarejea Syria kutokea London alipokuwa akiendelea na masomo yake na kujiunga na jeshi.
Bashar anajulikana kwa utawala wake wa ukandamizaji nchini Syria, ambayo tangu mwaka 2011 imeharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoangamiza nchi hiyo na kuifanya kuwa chimbuko la kundi la kigaidi la ISIS, huku ikisababisha vita vya kimataifa na mgogoro wa wakimbizi uliosababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.
Vita vilianza baada ya utawala wa Assad kukataa kusalimu amri mbele ya maandamano makubwa ya kudai demokrasia mwaka huo wakati wa Vuguvugu la Kiarabu (Arab Spring), badala yake ukachukua hatua kali dhidi ya harakati hiyo ya amani, ukiua na kuwafunga maelfu katika miezi ya mwanzo pekee.
Tarehe 8-12-2024 utawala wa Bashar pamoja na wa familia yake ukafikia kikomo baada ya ya utawala wa miaka 53 ya familia hiyo, ambapo Bashar aliripotiwa kukimbia baada ya Waasi kuudhibiti Mji wa Damascus alfajiri ya Desemba 8, 2024.
Uongozi wa Bashar ulifika kikomo baada ya kikundi cha waasi kuuteka mji wa Damascus na Kiongozi wa Waasi wa Kundi la Hayat Tahrir al-Sham, Abu Mohammed al-Julani alisema Taasisi zote za Serikali zitabaki chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu, Mohamed Ghazi al-Jalali kwa kipindi hiki.
Madai ya ndege ya Assad kudondoshwa
Zimekuwepo taarifa mbalimbali zikieleza kuwa ndege aliyoitumia Bashar kutoroka ilishambuliwa na hivyo kupelekea kifo cha Bashar akiwa katika jitahada hizo, tazama hapa na hapa.
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli kwani ufuatiliaji wa kimtandao umebaini kuwa Bashar alipokelewa na kupewa hifadhi yeye pamoja na familia yake huko Moscow Urusi ambapo vyombo mbalimbali viliripoti kuhusu suala hilo tazama hapa na hapa.