Inashangaza Kenya wanalalamika mambo ya Loliondo na wanahojiwa Aljazeera TV. Je, kuna mamluki Loliondo toka Kenya?

Inashangaza Kenya wanalalamika mambo ya Loliondo na wanahojiwa Aljazeera TV. Je, kuna mamluki Loliondo toka Kenya?

seedfarm

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
260
Reaction score
2,655
Taarifa ya Aljazeera TV imeambatanishwa kuhusu Wakenya wa Nairobi kutetea Loliondo kuwa Wamasai wabaki, Wakenya wa Nairobi wamewekeza kitu gani huko Loliondo?

Loliondo ni Tanzania wao Wakenya wanahojiwa na Aljazeera kuhusu sheria za ardhi Tanzania na wanapotosha kwa lengo gani?

Propaganda zinafanywa na Kenya kwa kiasi kikubwa kuharibu jina la Tanzania kimataifa, Loliondo ipo Tanzania kwa nini Wakenya wapo mbele kuelezea mambo ya Loliondo yasiyowahusu huko Aljazeera TV

Je, Wakenya wana maslahi na Loliondo?

Je, yale makundi ya mifugo Loliondo ina milikiwa na matajiri wa Kenya wa Nairobi ambao ndio wanahojiwa Aljazeera TV?

Ni Hakika kuna Wakenya wengi huko Loliondo.

Inashangaza Wakenya wa Nairobi ndio wanahojiwa na Aljazeera TV huku wakielezea kwa uchungu kuwa lazima wamasai wabaki Loliondo.

Wakenya wanasema kuna majeruhi katika hospitali za jirani walioumizwa na polisi.

Kwa nini wahojiwe Wakenya wa Nairobi na sio Watanzania wa Loliondo, Loliondo Itakuwa imevamiwa na Wakenya.

Ni wakati wa Serikali kuwa makini na wafugaji na watu toka Kenya waliojazana huko Loliondo.

Video Nimeambatanisha
 
Wanajua kutumia weakness katika uongozi wetu, usingewasikia wakati wa Magufuli.

Walikuja juu sana wakati wa Kikwete kwenye mradi wa barabara ya kutoka Arusha kwenda Musoma utadhani ilikuwa ndani ya mipaka yao. Yule jamaa marehemu alipoamua bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda Tanga, hawafuruka kabisa japopokuwa lilikuwa linapita maeneo hayo hayo waliyopigia kelele wakati wa Kikwete.
 
Kama una ushahidi wa mamluki wa Loliondo toka Kenya peleka ushahidi wako polisi, lakini kama unahisi kaa kimya.

Wakenya wana haki ya kupinga ukatili wanaofanyiwa wamasai wa Loliondo na serikali ya Tanzania, kama ambavyo wapenda haki duniani kote wanaruhusiwa.

Wewe huna haki yoyote ya kuwafunga midomo wakenya. Hakuna propaganda inayofanywa na wakenya kuharibu jina la Tanzania.

Jina la Tanzania linaharibiwa na serikali yetu wenyewe kwa ukatili wake kwa wananchi wake, yeyote anayekemea ukatili huo hawezi kuwa anaharibu jina la Tanzania.

Serikali ya kidikteta iliyovitisha vyombo vya habari kuripoti juu ya ukatili wanaofanyiwa wamasai wa Loliondo inastahili kukemewa sio na wamasai wa Kenya pekee, bali toka pande zote za dunia.
 
Serikali ya Tanzania walidhani kuzuia hizi local media za bongo hizi za njaa habari haitafika Duniani.

Ulimwengu huu wa kidigitali unazuia itv kama vile hao ndio wanaojua kupiga picha ama ndio peke yao wenye simu.

Habari imefika Duniani, royal tour imejifia kifo cha mende.
 
Ardhi yote ya Tanzania ni mali ya serikali ya Tanzania, watanzania wote hata wwnye hati miliki wanapangishwa ardhi na serikali, ndio maana kila mwaka tunalipa land rent serikalini.

Miradi mingi tu imepita maeneo ya watu, watu wanalipwa fidia na kuondoka, kama mradi hauhitaji fidia, watu wanaondoka tu.

Wamasai wasijidanganye ardhi hiyo ni yao, hawana umiliki wa hiyo ardhi, hivyo serikali kama imeona ardhi inafaa kwa jambo jingine inayouwezo wa kuwahamishia wamasai sehemu salama.
 
Waziri mkuu si alisema hali ni shwari na RC anatangaza kuuliwa kwa askari huku akiacha kutaja wananchi waliojeruhiwa mpaka hapa nikidhibitisho kuwa hakuna utetezi dhidi ya raia bali ni maslahi binafsi yamepewa kipaumbele!
 
Wewe Itakuwa mmasai

Jiwe limepigwa gizani

Ukisikia ohoooo ujue limekupata

Mbona watu walihamishwa kimara kupisha barabara?

Ardhi ni ya serikali Wataishi hapo kwa kuzaliana mpaka lini?

Hata kule kwenye migodi North Mara, kule kwenye gas Mtwara, inakopita SGR, orodha ni ndefu waliondolewa, lkn hata hatukusikia kelele kama hizi. Kwani wamasai ni akina nani mpaka wawe juu ya sheria?

Mbona wenyewe wako kila kona ya nchi. Sumbawanga, Lindi n.k. hakuna wanaowaghasi wala kuwabughudhi?
 
Wakenya huwa siwapendi kwa unafiki wao haswa linapokuja suala la maslahi.

Lakini kwenye hili wana haki ya kupiga kelele na serikali itambue upuuzi ilioufanya.

Kama serikali yetu na taasisi ya ulinzi imelala kiasi kwamba watu wanatoka nje ya nchi na kuingia, kujenga na kufuga, huku uongozi uko kimya...inabidi viongozi waendelee kunyamaza wakati hao wageni wanapotetea kile wanachoamini ni haki zao.
 
Hata kule kwenye migodi North Mara, kule kwenye gas Mtwara, inakopita SGR, orodha ni ndefu waliondolewa, lkn hata hatukusikia kelele kama hizi. Kwani wamasai ni akina nani mpaka wawe juu ya sheria??
Mbona wenyewe wako kila kona ya nchi. Sumbawanga, Lindi n.k. hajuna wanaowaghasi wala kuwabughudhi?
Yani hakuna kabila lilipewa upendeleo kama wamasai nchi hii, wamekaribishwa karibu kila mkoa na kutengewa maeneo ya kulishia mifugo yao, ila kutwa kucha wao ni ugomvi na wakulima, kulisha kwenye mashamba ya watu wao kwao ni sawa.

Hakuna mtu aliyejuu ya sheria.
 
Wakenya huwa siwapendi kwa unafiki wao haswa linapokuja suala la maslahi. Lakini kwenye hili wana haki ya kupiga kelele na serikali itambue upuuzi ilioufanya.

Kama serikali yetu na taasisi ya ulinzi imelala kiasi kwamba watu wanatoka nje ya nchi na kuingia, kujenga na kufuga, huku uongozi uko kimya...inabidi viongozi waendelee kunyamaza wakati hao wageni wanapotetea kile wanacoamini ni haki zao.
Acha dawa iwaingie, huwezi ingia ndani ya nchi ya mwenzako kinyemela kiasi hiko, alafu ukiambiwa toka ulete vurugu, it might be seen kwamba hao jamaa wanaonewa, ila kiuhalisia hakuna anayeonewa.
 
Back
Top Bottom